.

.
Monday, November 12, 2012

8:52 AM
 
Mbowe akihutubia mkutanoMWENYEKITI  wa  Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe, amemtaka Waziri Mkuu, mstaafu Fredricke Sumaye, kujiondoa CCM na kujiunga na Chadema, bila masharti ya kuteuliwa na chama hicho kugombea urais mwaka 2015.

Akizungumza katika mkutano mkubwa katika mji wa Katesh ambako ni nyumbani kwa Sumaye na Nagu, Mbowe alisema anashangazwa na Sumaye kuendelea kulalamikia rushwa iliyosababishia kushindwa kupata ujumbe wa Halmashauri Kuu ya (NEC) kupitia Wilaya ya Hanang.

Katika mkutano, mamia ya wafuasi wa Sumaye, wakiwemo wazee maarufu wa CCM katika Kata ya Endasaki, wajiunga na Chadema.

Wafuasi hao ni wale waliokuwa wakipinga Dk Nagu kupambana na Sumaye katika kuwania ujumbe wa NEC.
Katika hotuba yake, Mbowe alisema Sumaye  ndiye alimlea Dk Nagu bila kujua anafuga mzimu ndani ya nyumba yake 
Baada ya matokeo ya NEC Hanang , nilimpigia simu Sumaye nikamweleza tayari ameshindwa na anachopaswa kufanya ni kuvua gamba na kuvaa gwanda na sio kuendeleza malalamiko ya kushindwa.............. alisema Mbowe.

0 comments:

Post a Comment