.

.
Wednesday, November 7, 2012

1:15 AM




 Kanisa katoliki tanzania limepata pigo kwa kifo cha Mhashamu askofu Aloysius Balina (pichani), Askofu wa Shinyanga, kilichotokea katika hospitali ya Bugando jijini Mwanza tarehe 6 Novemba, 2012 saa tano asubuhi. Alikuwa na saratani. 
Mazishi yanatarajiwa kufanyika  Shinyanga Jumamosi tarehe 10 Novemba, 2012. 
Mhashamu askofu Aloysius Balina, alizaliwa Juni 21,1945, Ntuzu, Bariadi mkoani Shinyanga, Upadre mwaka 1971 na  alikuwa askofu mwanzilishi wa jimbno la Geita mwaka 1985, na baadaye akateuliwa kuwa askofu wa Shinyanga mwaka 1997. 
Kwa zaidi ya miaka 20 amesimamia shughuli za kanisa Katoliki katika idara ya afya, akiwa vile vile mwenyekiti wa bodi ya hospitali ya rufaa ya Bugando. Yeye ndiye mwanzilishi wa Chuo Kikuu cha Tiba cha Bugando.
Marehemu  alizaliwa Juni 21,1945, Ntuzu, Bariadi mkoani Shinyanga, Upadre mwaka 1971 na  alikuwa Askofu mwanzilishi wa jimbo la Geita mwaka 1985, na baadaye akateuliwa kuwa askofu wa Shinyanga mwaka 1997. 
Kwa zaidi ya miaka 20 amesimamia shughuli za kanisa Katoliki katika idara ya afya, akiwa vile vile mwenyekiti wa bodi ya hospitali ya rufaa ya Bugando. Yeye ndiye mwanzilishi wa Chuo Kikuu cha Tiba cha Bugando.
Mhashamu askofu Aloysius Balina enzi za uhai wake akiwa na Rais Jakaya Kikwete katika moja ya shughuli za Hopsitali ya Bugando, Mwanza

Mhashamu askofu Aloysius Balina enzi za uhai akihutubia  
Mhashamu askofu Aloysius Balina  akisalimiana na Laurean Kardinal Rugambwa enzi za uhai wao, na sasa wote wametangulia mbele za haki
.
BWANA AMETOA, BWANA AMETWAA, JINA LAKE LIHIMIDIWE
AMINA.........

0 comments:

Post a Comment