.

.
Thursday, November 22, 2012

9:14 PM

Mapigano yaendelea Gaza

Mapigano yameendelea usiku kucha katika eneo la Gaza licha ya fununu kuwa kumewekwa mkataba wa kusitisha mashambulio.
Israel inadaiwa kuendeleza mashambulio hayo katika maeneo kadhaa ya Gaza yaliyosababisha kupoteza kwa nguvu za umeme.
Takriban wapalestina ishirini wameripotiwa kuuawa .
Hapo jana Israel ilisambaza ilani kuwaonya wakaazi waliokuwa pembezoni mwa Gaza, wahamia katikati mwa jiji kwa usalama wao.
Isarel imesema kuwa wapiganaji wa kipalestina wamerusha zaidi ya makombora mia na hamsini kwenye ardhi yake tangia Jumanne.
                            .......XXX...............XXX...........XXX

Mkewe Gbagbo kufikishwa the Haque

Simone Gbagbo
Simone Gbagbo
Mahakama ya kimataifa ya Jinai ICC, imetoa kibali cha kukamatwa kwa mke wa aliyekuwa rais wa Ivory Coast Laurent Gbagbo, Bi Simone, Gbagbo.
Bi Gbagbo anasakwa kwa tuhuma za kuhusika na uhalifu wa kivita wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyoibuka baada ya uchaguzi wa urais nchini humo.
Mumewe tayari amekamatwa na anasubiri kesi yake kuanza katika mahakama hiyo iliyoko The Haque, kuhusiana na madai hayo ya uhalifu wa kivita.
Takriban watu 3,000 waliuawa kwenye machafuko yaliyotokea baada ya ya Gbagbo kukataa kukubali matokeo ya uchaguzi wa Urais.
Gbagbo na mkewe walikamatwa ndani ya handaki moja Aprili mwaka wa 2011, miezi mitano, baada ya uchaguzi wa urais.
Wanajeshi wa rais wa sasa wakiungwa mkono na wanajeshi wa Umoja wa Mataifa walianzisha msako mkali dhidi yao, baada ya kujificha ndani ya ikulu ya rais.
anatuhumiwa kuhusika na mauaji, ubakaji, dhuluma na ngona na kuwadhulumu wapinzani wa serikali miongoni mwa mashtaka mengine mjini Abidjan.
Licha ya kuwa Bi Gbagbo hakuwa akiwania kiti chochote cha kisiasa, ripoti zinasema kuwa alikuwa na mamlaka makubwa na kuwa alimshawishi mumeo kutokubali matokeo ya uchaguzi.
Gbagbo, 67, alihamishwa hadi The Haque mwaka uliopita, na kuandikisha historia ya kuwa rais anayeondoka wa kwanza kufikishwa mbele ya mahakama hiyo ya ICC.
Rais huyo wa zamani amekanusha madai hayo yote.
Kabla ya kuhamishwa hadi the Haque, Gbagbo na mkewe mwenye umri wa miaka 63, walifunguliwa mashtaka nchini Ivory Coast kuhusiana na uhalifu wa kiuchumi, ikiwemo mdai ya kupora mali, wizi wa nguvu na kutumia rasilimali za umma kwa njia mbaya
Mahakama hiyo ya ICC sasa imetoa wito kwa serikali ya Ivory Coast, kumusafirisha Bi Gbagbo ili afunguliwa mashtaka huko the Haque.
                           .........xxx...........xxx............xxx.............

Jaribio la mapinduzi yatibuliwa Sudan

Salah Gosh
Salah Gosh
Watu kadhaa wamekamatwa na serikali ya Sudan, wakiwemo mkurugenzi mkuu wa zamani wa idara ya ujasusi, Salah Gosh na maafisa kadhaa wa jeshi la nchi hiyo kufuatia madai ya kujaribu kupindua serikali ya nchi hiyo.
Raia kadha wamesema wameona magari kadhaa ya kivita na wanajeshi wakishika doria katika barabara za mji mkuu wa nchi hiyo Khartoum.
Katika miezi ya hivi karibuni, Utawala wa Khartoum umeshuhudia kuongezeka kwa maandamano dhidi ya serikali, kupinga kuongezeka kwa bei ya chukula na pia kushinikiza mabadiliko ya kisiasa.
Rais wa Sudan Omar al-Bashir amekuwa madarakani tangu mapinduzi ya serikali mwaka wa 1989.
Waziri wa habari wa Sudan Ahmed Belal Osman, amesema watu 13, wamekamatwa kuhusiana na njama hiyo ya kupindua serikali.
chanzo:bbc

0 comments:

Post a Comment