.

.
Wednesday, November 7, 2012

9:50 PM
Aliyekuwa m'bunge wa jimbo la Arusha mjini Godbless Lema akihutubia katika moja ya mikutano yake jijini Arusha
USIKILIZWAJI wa uamuzi wa pingamizi za awali wa kesi ya rufaa iliyofunguliwa na aliyekuwa mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema, (CHADEMA), leo kujulikana hatma yake.
 Rufaa hiyo inayotarajiwa kusikilizwa mapema leo hii jijini Dar, na majaji watatu wakiongozwa na Jaji Mkuu, Mohamed Othman Chande, Natalie Kimaro na Salum Massati itatoa maamuzi (hatma) juu ya ubunge wa aliyekuwa mbunge wa jimbo la Arusha mjini Godbless Lema.
Awali kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Naibu Msajili wa Mahakama, Maximilan Malewo, uamuzi wa pingamizi hizo ulipangwa kutolewa Novemba 29 mwaka huu jijini Dar es Salaam.
Lema akiwajulisha wafuasi wa CHADEMA (hawapo pichani) juu ya uamuzi wa mahakama kuhamishia rufaa hiyo jijini Dar mara baada ya kutoka kusikiliza rufaa hiyo octoba 2 mwaka huu
Ingawa wakati Jaji Mkuu Chande akiahirisha shauri hilo jijini Arusha octoba 2 baada ya kusikiliza hoja za pingamizi kutoka kwa mawakili wa wajibu rufaa na majibu toka kwa mawakili wa mleta rufaa, alisema uamuzi huo ungetolewa Oktoba wakati wa vikao vya mahakama hiyo.


0 comments:

Post a Comment