.

.
Sunday, November 18, 2012

10:50 AM

 Waziri wa Sayansi Mawasiliano na Technojia Prof. Makame Mbarawa akifungua jiwe la msingi kuashiria uzinduzi rasmi wa radio ya jamii ya LOLIONDO FM wakati wa hafla maalum ya uzinduzi wa radio kijijini Ololosokwani. Uwekwaji wa redio hiyo  ya jamii umezeshwa kwa ushirikiano kati ya Airtel na shirika lisilo la kiserikali UNESCO katika kijiji cha Ololosokwani kilichopo Loliondo Wilayani Ngorongoro Mkoani Arusha. Kulia ni mkurugenzi wa mawasiliano wa Airtel Bi, Beatrice Singano na wakwanza shoto muwakilishi wa UNESCO bi Vibeke Jensen
 Waziri wa Sayansi Mawasiliano na Technojia Prof. Makame Mbarawa akijaribu mtambo wa radio kwa kutangaza moja kwa moja (live) kupitia radio ya jamii LOLIONDO FM mara baada kumalizika kwa  hafla ya

uzinduzi rasmi  wa radio hio ya jamii iliyowezeshwa kwa ushirikiano kati ya Airtel na shirika lisilola kiserikali UNESCO katika kijiji cha Ololosokwani kilichopo Loliondo Wilayani Ngorongoro Mkoani Arusha. Waliomzunguka wawakilishi  Airtel na Unesco wakiwa na wenyeji wa kijiji cha Ololosokwani

Picha Waziri wa Sayansi Mawasiliano na Technojia Prof. Makame Mbarawa akitoa wito kwa wanafunzi na wanakijiji wa Ololosokwani  kuhakikisha wanatumia vyema kituo cha mtandao wa Internet (multi media center) katika shughuli za masomo yao mara baada ya waziri huyo kuzindua mradi wa radio ya jamii LOLIONDO FM, mradi wa mtandao pamoja na kampeni ya kuwafundisha jamii ya wamasai kujenga nyumba za kisasa katika kijiji cha Ololosokwani kilichopo Loliondo Wilayani Ngorongoro Mkoani Arusha. Waliomzunguka wawakilishi  Airtel na Unesco wakiwa na wenyeji wa kijiji cha Ololosokwani

0 comments:

Post a Comment