.

.
Wednesday, November 14, 2012

10:35 AM

Naibu Katibu Wakuu, Mwigulu Nchemba (Bara),Na Mwandishi Wetu,Dodoma
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimeanza harakati za kutafuta uungwaji mkono kutoka umma wa Wataznania baada ya kuingiza sura mpya za
wanaoaminika kupinga ufisadi katika safu ya juu ya uongozi.

Miongoni mwa sura zinazoonekana kama kete ya CCM kwenye uchaguzi Mkuu ujao 2015 ni pamoja na Makamu Mwenyekiti Taifa, Phillip Mangula (Bara)
na Katibu Mkuu mpya, Abdulrahaman Kinana.

Licha ya kuongoza mikakati, kampeni na harakati za chaguzi za mwaka 2000 na 2005, Kinana na Mangula wanatajwa kuwa miongoni mwa wana CCM
wachache wanaoendelea kuamini katika misingi ya chama hicho kwa kupinga ufisadi, rushwa na mambo yote yanayokiuka maadili ya uongozi.

Ni Mangula aliyeongoza harakati za kuwadhibiti wana Mtandao wakati wa zoezi la kura za maoni ndani ya CCM mwaka 2005 kwa kuwatuma wajumbe wa
kamati ya maadili chini ya Kanali Mhando na Paul Sozigwa kuzunguka nchi nzima kukusanya taarifa na nyaraka ambazo zingetumika kumuengua
Jakaya Kikwete katika kinyang’anyiro, kabla ya Mwenyekiti Mstaafu Benjamin Mkapa kuweka pembeni taarufa hiyo.Katibu Mkuu mpya, Abdulrahaman Kinana.

Kwa upande wa Kinana, huyu ndiye mjumbe wa NEC na CC ya CCM aliyetoa hoja ya kuvunjwa kwa Kamati Kuu ya Chama hicho kutoa fursa kwa
Mwenyekiti, Rais Kikwete kuusuka upya na hivyo kuwaondoa akina Andrew Chenge, Rostam Aziz na wengine kadhaa.

Katika kikao hicho ndimo kauli mbiu ya kujivua gamba lilipoibuka likiwalenga watuhumiwa wa ufisadi ulioshuhudia Rostam akijivua
nyadhifa zote ndani ya chama na kubaki kuwa mwanachama wa kawaida huku Chenge na Lowassa waliokuwa wakitajwa wakigoma kuachia nyadhifa zao.

Baadaye Lowassa alikaririwa kwenye moja ya vikao vya NEC kumshutumu Mwenyekiti wake kwa kuruhusu wajumbe wa sekretarieti ya CCM, akiwemo
Nnape Mnauye kuzunguka nchi nzima kumtangaza kama gamba linalotakiwa kuvuliwa ndani ya chama.

Safu nzima ya sekretarieti mpya ya CCM iliyopitishwa na NEC mjini Dodoma ni pamoja na Manaibu Katibu Wakuu, Mwigulu Nchemba (Bara), Vuai
Ally Vuai (Zanzibar), Zakia Meghji (fedha na uchumi, Mohamed Seif Hatib (Oganaizesheni), Dk Asha Rose Migiro (Mahusiano ya Nje) na
Mnauye anayeendelea kutamba kwenye Itikadi na Uenezi.

0 comments:

Post a Comment