.

.
Friday, November 9, 2012

4:03 PM

Salma Yusufu

Walter Chilambo ambaye ndiye aliyeshinda kitita cha shilingi milioni 50 za EBSS

Shindano la EBSS usiku huu limefikia patamu baada ya washiriki 3 walio ingia katika fainali hizo kutoka na sasa kubakia washiriki wawili ambao ni Walter Chilambo na Salama Yusufu mwakilishi pekee kutoka kisiwani Zanzibar. Na Hatimaye WALTER kuibuka kidedea.
Washiriki waliotoka usiku huu na kuachia kitita chaa Shilingi Milioni 50, kikiwaniwa na Walter na Salama ni pamoja na Nsami Nkwabi, Nshoma Ng’hangasamala Wababa Mtuka.
Shindano la EBSS linafikia tamati yake usiku huu katika ukumbi wa Diamond Jublee linapoendea kufanyika.

Kama kawaida nao hutoa burudani ....Chief Jaji na mratibu wa Shindano la Epiq Bongo Star Search (EBSS), Mkurugenzi wa kampuni ya Benchmark Productions Limited, Ritha Poulsen a.k.a Madam Ritha, akifurahia jambo wakati washiriki wakitumbuiza jukwaani. Kulia ni Jaji mwingine Master Jay akionekana kama kukera na kicheko cha Madam Ritha.

Mashabiki na wapenzi wa shindano la Epiq Bongo Star Search (EBSS) waliofurika katika ukumbi wa Diamond Jubelee wakilipuka kwa shangwe baada ya mmoja wa washiriki ambao wanamkubali kumaliza kufanya show yake.
MC’s wa Show hii ya leo ni kijana mtanashati Caesar Daniel na mwana dada mrembo Vanessa Mdee ndio wanasongesha show nzima ya leo.
Huyu ni Salama Jabir na hapa ni katika yale ya Look ndani ya fainali za EBSS 2012

Washiriki wa Washindano la EBSS 2012 ambao wamefanikiwa kuingia fainali ya shindano hilo wakiwa jukwaani usiku huu wakati wa kuanza kwa fainali hizo. ndani ya Ukumbi wa Diamond Jijini Dar es Salaam. usiku wa leo

0 comments:

Post a Comment