Rais
wa Marekani,Barack Obama akiwahutubia wananchi wa Marekani mara baada
ya kutangazwa ni mshindi katika Uchaguzi Mkuu wa nchi hiyo,dhidi ya
Mpinzani wake,Mitt Romney.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete
ameeleza furaha na shangwe yake kufuatia ushindi wa jana, Jumanne,
Novemba 6, 2012 wa Rais Barack Obama wa Marekani katika Uchaguzi Mkuu
wa nchi hiyo.
"Nimepokea kwa furaha na shangwe
habari za kuchaguliwa tena kwako kuwa Rais wa Marekani kwa kipindi cha
pili. Kwa niaba ya Serikali na Wananchi wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, na kwa hakika, kwa niaba yangu mwenyewe, napenda kukutumia
wewe na kupitia kwako Chama cha Democratic pongezi nyingi kwa ushindi
wako wa maana sana.” amesema Rais Kikwete katika taarifa ya Ikulu
iliyotumwa leo.
"Kuchaguliwa kwako tena
kuendelea kuongoza nchi yako muhimu na wananchi wake, ni ishara ya wazi
ya uaminifu na imani ambayo wananchi wa Marekani wanayo katika uongozi
wako wa mfano.” Rais kikwete amesema katika salamu zake hizo, na
kuongeza:
"Wakati unajiandaa kuchukua tena
uongozi wa nchi hiyo katika kipindi chako kipya, napenda kukuhakikishia
msimamo wangu binafsi na ule wa Serikali yangu kuwa tutaendelea kufanya
kazi kwa karibu kabisa na wewe na Serikali yako ya kutukuka, ili
kuendeleza uhusiano bora ulioko kati ya nchi zetu mbili ndugu.”
0 comments:
Post a Comment