.

.
Thursday, November 15, 2012

9:37 AM

Mshambuliaji Bafetimbi Gomis wa Ufaransa (18), akishangilia bao lake alilofunga dhidi ya Italia. Ufaransa ilishinda 1-0 katika pambano hilo jijini Parma, Italia.

PARMA, Italia
Zikicheza bila wachezaji wake muhimu na mihimili, Uholanzi na Ujerumani zilimaliza dakika 90 kwa sare isiyo ya mabao ndani ya dimba la Amsterdam ArenA
TIMU ya taifa ya Ufaransa, imeendelea kuimarisha kiwango chake dimbani ilichoonesha katika sare ya 0-0 dhidi ya Hispania hivi karibuni, ambapo usiku wa kuamkia leo iliibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Italia, shukrani kwa bao la mtokea benchi Bafetimbi Gomis.

Stephan El Shaarawy alifunga bao la uongozi kwa Italia kipindi cha kwanza, lakini Mathieu Valbuena akaifungia Ufaransa bao la kusawazisha, kabla ya Gomis kufunga la ushindi akimalizia krosi ya Patrice Evra kipindi cha pili.

Mabao sita yalitinga nyavuni katika pambano la kuvutia jijini Stockholm, katika pambano baina ya wenyeji Sweden waliobebwa na mabao ya Zlatan Ibrahimovic katika ushindi wa 4-2 dhidi ya kikosi cha England chini ya kocha Roy Hodgson.

Mabao kutoka kwa Danny Welbeck na Steven Caulker yaliashiria mwanzo mwema wa mechi ya kirafiki, lakini Ibrahimovic akaonesha namna alivyo hatari kwa kufunga mara nne, ikiwamo ‘tik-tak’ maridadi mwishoni mwa pambano hilo kuipa ushindi mnono nchini yake.

Zikicheza bila wachezaji wake muhimu na mihimili, Uholanzi na Ujerumani zilimaliza dakika 90 kwa sare isiyo ya mabao ndani ya dimba la Amsterdam ArenA.

Mesut Ozil, Mario Gomez na Bastian Schweinsteiger yalikuwa miongoni mwa majina makubwa ya Ujerumani yaliyokosa mechi hiyo, kama ilivyokuwa kwa Robin van Persie na Wesley Sneijder waliokosekana kwa upande wa Uholanzi.

MATOKEO YA MECHI NYINGINE DUNIANI
NOVEMBA 15, 2012                       
Honduras 0 - 0 Peru
Venezuela 1 – 3 Nigeria
Bolivia  1 – 1 Costa Rica
Brazil 1 – 1 Colombia

NOVEMBA 14, 2012           
Panama 0 – 3 Hispania
Italia 1 – 2 Ufaransa
Ireland  Kaskazini 1 – 1 Azerbaijan
Jmahuri ya Ireland 0 – 1 Ugiriki
Poland  1 – 3 Uruguay
Albania 0 – 0 Cameroon
Gabon  2 – 2 Ureno
Austria 0 – 3 Ivory Coast
Sweden 4 – 2 England
Uholanzi 0 - 0   Ujerumani
Luxembourg 1 – 2 Scotland
Uturuki 1 – 1 Denmark
Romania 2 - 1  Ubelgiji
Morocco 1 – 1 Togo
Chile 1 – 3 Serbia
Cape Verde 0 – 1 Ghana
Israel 1 – 2 Belarus

0 comments:

Post a Comment