.

.
Friday, November 9, 2012

2:49 PM

Askofu mpya wa Anglikana Justin Welby (kulia)

Aliyetangazwa kuwa askofu mkuu wa kanisa Anglikana Cantebery na ambaye amethibitishwa hii leo, Justin Welby amesema ameshangazwa sana na wadhifa aliopewa wa kuliongoza kanisa hilo.
Katika mkutano na waandishi wa habari, Askofu Justin Welby ambaye ni askofu wa Durham, alielezea msimamo wake wa kuunga mkono kutawazwa kwa wanawake kama maaskofu.
Aliongeza kuwa watu watu hawapaswi kuwanyanyapa wapenzi wa jinsia moja kanisani, lakini akakiri kuna mgawanyiko kanisani kuhusu ndoa za jinsia moja.
Welby aliyefanya kazi katika sekta ya mafuta , anaonekana kama mhafidhina kwa mrengo wa kanisa hilo ambalo linaegemea upande wa kiivanjelisti. Ataanza kazi yake mwezi Machi mwaka ujao baada ya Askfo mkuu Rowan Williams kuachia ngazi.
Baada ya uteuzi wa Askofu mkuu Justin Welby kuwa mkuu wa Kanisa la Anglikana, viongozi mbalimbali wa kanisa hilo wamezungumzia uteuzi huo.
 Baadhi ya maaskofu wa nchi mbali mbali wa makanisa ya  Kianglikana akiwemo wa Nigeria na Tanzani askofu Mokiwa wamepinga vikali kanisa kutetea mapenzi ya jinsia moja

0 comments:

Post a Comment