.

.
Monday, November 12, 2012

9:01 PM

Hii ni kejeli......, miaka 50 ya uhuru bado kuna watanzania wanaishi maisha ya binadamu wa kale huku kauli mbiu ya maisha bora kwa kila mtanzania ikishika hatam, Je, maisha bora kila mtanzania ni yapi.....? mbona kwa matendo ni "maisha bora kwa baadhi ya watanzania"? hasa kwa baadhi ya wenzetu wa jamii ya wahadzabe?

Mkazi wa kitongoji cha Kipamba kata ya Mwangeza ambaye amekataa kutaja jina lake akiwa kwenye nyumba yake ya kuishi na familia yake.  
 Mkazi wa kitongoji cha Kipamba kata ya Mwangeza wilaya ya Iramba ambaye hakuweza kujulikana jina lake mara moja akiomba alipwe fedha za kumpiga picha. 

 Hadza au Wahadzabe ni kabila linaloishi Kaskazini ya Kati Tanzania wanoishi kuzunguka Ziwa Eyasi eneo la Karatu, Mkoa wa Manyara, pia wanapatikana Mbulu, Iramba, Meatu na Maswa. Kabila hilo ni jamii pekee nchini Tanzania inayoishi kwa kutumia mfumo wa binadamu wa kale ambapo wanaishi kwa kutegemea uwindaji pamoja na kukusanya mizizi na matunda ya pori kama chakula kikuu hadi leo hii Tunaposheherekea miaka 50 ya uhuru.

Tofauti na makabila mengine ambayo yanajihusisha na kilimo, ufugaji, uvuvi, biashara na shughuli mbalimbali za kuingiza kipato, shughuli kubwa ya wanaume wa Kihadzabe huwinda kwa kutumia upinde na mshale. Wanawake wanajihusisha na ukusanyaji wa mboga, mizizi na matunda pori kisha kukusanyika pamoja na kula kisha kukaa kwa ajili ya kusubiri kesho bila kujua siku,tarehe wala mwaka.

Wanawake wa Kihadzabe wakishamaliza kukusanya mizizi na matunda, hugonga na kusaga mbegu za ubuyu kisha kutumia unga wake kutengenezea uji. Wakati wanaume hutumia muda wao kutengeneza upinde na mishale.

Kwa kifupi kabila hilo halijui thamani wala karaha ya kukosa fedha kwa sababu linaishi maisha ya kipekee katika maeneo ya nyikani ambapo hakuna matumizi ya kujenga nyumba, samani za ndani, kununua nguo, chakula wala gharama za matibabu ambapo hutegemea mizizi kwa matibabu pia hawana makazi ya kudumu.

Wakati watanzania wakiahidiwa maisha bora kwa kila mtanzania siku zote za maisha ya kila siku, jamii hii huahidiwa nyakula na vinywaji kipindi cha sensa tu ili wakubali kuhesabiwa na baada ya kuhesabiwa habari yao imeishia hapo.

Nakusudia kusema kuwa jamii hii imekuwa kama chambo tu ya kuongeza idadi ya watanzania ili zipatikane fedha za kufanyia shughuli mbalimbali, kwani mbali na kesabiwa..., kuletewa maendeleo kama ilivyo lengo la sensa kwao ni ndoto bali huishia kutelekezwa.

Bw.Abel Matayo, mkazi wa kitongoji Kipamba, kata Mwangeza, Iramba, wa
jamii ya Kihadzabe akiaga familia tayari kwa safari kuwinda
 Mmoja wa Wahadzabe, Abel Matayo akivuta sigara nyumbani kwake Kipamba, kata Mwangeza kabla ya kuelekea kuwinda porini.

Kuna baadhi ya watu wanajitahidi sana kupotosha umma kwamba jamii hii haihitaji maendeleo ya kujengewa barabara kuacha kutembea maporini, shule kwani wao hata hawajiu kama kuna kusoma, soko ili kujichanganya na watu na kuacha kutegemea mawindo, hospitali na kuacha kutegemea mizizi pekee.

Aidha jamii hii kwa sasa wamefanywa kama sehemu ya utalii kwa wenzetu wazungu kwa kisingizio kuwa wale ni mabaki ya binadamu wa kale kutokana na fuvu la mtu wa kale kupatikana kwa jamii hiyo

viongozi wetu wa vyama vyote hamjui kama kuna watu hawa.........?na wao wana mahitaji ya MAISHA BORA KWA KILA MTANZANIA..? kwani jamii hii inaishi pembezoni mwa baadhi ya viongozi wetu wa vyama vyotehicyo hakuna wa kusema hajui kama kuna hilina kama yupo......AJITOKEZA KUNIJULISHA NIMPELEKE.
 

0 comments:

Post a Comment