.

.
Sunday, November 11, 2012

5:46 AM

Fadhili Mwasyeba, Meneja wa Zuku Tanzania (katikati) akizungumza na Waandishi wa HabariNovemba 9, 2012. Kipindi maarufu cha "Hyped East Africa Show" kinachorushwa na kingamuzi cha Zuku Pay TV wanaendelea kutafuta klabu bora Afrika Mashariki, imemleta DJ Nijo kupiga shoo kali kwenye kumbi maarufu jijini Dar es Salam. John Waititu aka Dj Nijo alingia Dar es Salaam jana, ijumaa na
kesho Jumamosi watafanya shoo Bilicanas.
 Akizungumza na waandishi wa habari, John Waititu aka Dj Nijo alisema "Ninayofuraha kurudi Dar Es Salaam kwajili ya kuendelea kutafuta klabu bora Afrika Mashariki. Tulivo tembelea Dar Es Salaam mara ya mwisho, mashabiki walipenda shoo ilibidi turudi tena.
 Pia aliongezea " Jumamosi hii tutakuwepo Saturday Night Fever na tutakuwa na DJ's Ibra, Paul and Ejay. Aliwakaribisha watu wote kuja klabu Bilicanas kuwakilisha jiji lao, ili ichaguliwe kuwa klabu bora Afrika Mashariki."
 Timu ya Hyped East Africa wanategemea wasanii wabongo kuwepo kwajili ya kuwafanyia intaviu ambayo itaonyeshwa kwenye shoo ya Hyped East Africa ya Zuku Afrika.John Waititu aka Dj Nijo
 Akiongea na wandishi wa habari, Fadhili Mwasyeba, Meneja wa Zuku Tanzania alisema " Zuku inaendelaa kuwekeza nchini Tanzania, na ujio wa Dj Nijo kwa mara ya pili ni moja kati ya ahadi zetu. Na siku ya Jumamosi tunataka watu kuja kwa wingi kwajili yakuwakilisha jiji la Dar es Salaam hapo club Bilicana."
 Aliongezea pia kuwa kwenye shoo hii, kutapambwa na ubora wa hali ya juu na wengi watasuuzika kwa kushuhudia shoo hiyo ambayo imekuwa ikiacha gumzo kila jiji anazopiga shoo DJ Nijo zikiwemo ndani ya Afrika Mashariki. Pia watu watapata nafasi kupiga picha na masupa star na kujishindia zawadi.
 DJ Nijo yuko kwenye ziara ya kupiga shoo kwenye klabu maarufu za miji mikubwa ndani ya Afrika Mashariki na vipindi vyote vya Hyped East Africa vinarushwa Zuku Afrika kila jumamosi saa 3:30 usiku.
 Shoo ya "Hyped East Africa" imefanywa Kampala (Cayenne Club & Anjenoir (Gavuno) club), Dar es Salaam ( Nyumbani Lounge & Club Sun Cirro), na mijik megine 8 hapo Kenya.

0 comments:

Post a Comment