.

.
Friday, November 2, 2012

1:46 AM
Jana Rais Kikwete alisubiriwa kwa mabango njiani na watoto wa shule ya msingi iliyoko wilayani Arumeru kutaka kuomba kurudishiwa shamba lao la shule wanalolitegemea kwa chakula lililoperwa na muwekezaji na kuzungushia fensi pamoja na kumwaga material kutaka kujenga



Wanafunzi wa shule ya mringa wakiwa njiani wanamsubiri rais kikwete kuwasilisha kilio chao cha kurudishiwa shamba la shule lenye eka 4 lililochukuliwa na mwekezaji huku wao wakikosa chakula
wanafunzi wa kiwa na mabango barabarani wakimsubiri Rais kumlilia juu ya shamba lao  lililochukuliwa na mwekezaji huku wanalindwa na polisi mkoani Arusha

Wakiongea na waandishi wa habari juu ya uamuzi wao wa kukaa barabarani kumsubiri Rais kuja kuwasikiliza mmoja wa wanafunzi hao alisema kuwa awali shamba hili lilikuwa likiwasaidia kupata chakula cha mchana shuleni kutokana na kulima wenyewe lakini tangu shamba hilo lichukuliwe na muwekezaji huduma ya chakula hakuna tena.

waliendela kusema kuwa viongozi wa serikali kuanzia ngazi ya kata na vijiji wameshindwa kutoa maelezo ya kutosha juu ya umiliki wa shamba la shule na muwekezaji huyo  hivyo wanamuomba Rais Kikwete kuwasaidia kulirudisha ili kusaidia kupanda kwa kiwango cha taaluma kwao kwa kutulia kusoma kwa kupata chakula shuleni

Haya ni baadhi ya mabango yaliyokuwa yameshikwa na wanafunzi hao kutoa ujumbe kwa Rais 

Hata hivyo pamoja na juhudi zao za kumsubiri Rais kupita na msafara wake ili kuelezea kilio chao, juhudi hizo ziligonga mwamba baada ya Msafara wa Rais kuchelewa, hivyo kuwapita bila kuwasikiliza.

0 comments:

Post a Comment