.

.
Tuesday, October 23, 2012

11:23 AM
KAMANDA WA POLISI MKOA WA ARUSHA, LIBERATUS SABAS ALIPOKUWA AKIONGEA NA WAANDISHI WA HABARI (HAWAPO PICHANI) OFISINI KWAKE
Mtu mmoja aliyejulikana kwa jina la Jumanne Kombo(28) mkazi wa Shamsi amefariki dunia jana usiku baada ya pikipiki aliyokuwa akiendesha kugongana uso kwa uso na gari aina ya Suzuki Escudo eneo la Philips darajani, barabara ya Arusha-Moshi Mkoani Arusha

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Kamanda wa polisi mkoa wa Arusha Liberatus Sabas alisema kuwa tukio hilo limetokea usiku wa saa 4:30 ambapo gari hilo lenye namba za usajili T. 474 ANF Lilikuwa likiendeshwa na mtu ambaye hajaweza kufahamika kwa haraka baada ya kukimbilia kusikojulikana.

Kamanda Sabas alisema kuwa chanzo cha tukio ni gari hilo aina ya Suzuki lilikuwa likitokea mjini kuelekea kimandolu kupasuka tairi la upande wa kulia na kuanza kuyumba na kuelekea upande wa pili wa barabara ambapo lilikutana uso kwa uso na pikipiki hiyo iliyokuwa ikitokea kimandolu kuelekea mjini.

Aidha Kamanda Sabas alisema kuwa pikipiki hiyo aina ya king lion lenye namba za usajili T. 920 BUA baada ya kugongana uso kwa uso na gari hilo, dereva(Jumanne)alifariki papohapo na dereva wa gari kukimbia ambapo jeshi la polisi linaendelea kumsaka na akipatikana atafikishwa katika vyombo vya sheria na mwili wa marehemu umehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali ya mkoa Mount Meru.

0 comments:

Post a Comment