.

.
Wednesday, October 17, 2012

6:58 AM

Hatimaye serikali imeamua kuwachukulia hatua za kisheria watu wanaohujumu utekelezaji wa mradi wa maji wa kijiji cha Laroi kilichoko katika kata ya Mateves Wilayani Arumeru.

Akitekeleza zoezi hilo Afisa Tarafa ya Mukulat Isack Kaserian Maroseck alitoa amri ya kukamatwa kwa mzee Rorian Mesheikini baada ya mzee huyo anayetuhumiwa kuongoza mgomo huo wa uchangiaji wa mradi wa maji na uharibifu wa miundombinu ya maji, kukaidi kuhudhuria kwenye kikao cha mazungumzo na viongozi mbalimbali ngazi ya kata na tarafa ili kumaliza mgogoro huo.

Mkutano huo ulioitishwa na afisa tarafa hiyo kwa niaba ya mkuu wa wilaya ya Arumeru Nyerembe Munassa siku ya jumatano katika ofisi ya kijiji cha Laroi kilimtaka mzee Mesheikini kuhudhuria mkutano huo kutoa malalamiko yake juu ya mgomo huo wa kuchangia mradi huo wa maji utakaokuwa ukombozi na msaada mkubwa kwa wananchi wa eneo hilo lakini alikataa ndipo Afisa huyo kutoa amri ya kwenda kukatwa kwa mzee huyo na polisi.

Aidha mzee Mesheikini na mwenzake ambaye hakuweza kufahamika kwa haraka walikamatwa na jeshi la polisi oktoba 10 na kupelekwa katika kituo kidogo cha polisi usa river huku wengine 12 wakiendelea kutafutwa kwa tuhuma za kukaidi amri ya kikao cha tarehe 29 agost ya kwenda kurejesha miundo mbinu yote ya maji waliyoharibu.

Isack alisema kuwa Kikao hicho cha tarehe 29 kiliwahusisha polisi, viongozi wa tarafa ya mukulat na kata zote za Tarafa hiyo, viongozi wa mradi na wananchi wote kwa ujumla na kujadili msaada wa mradi huo ambapo wote kwa pamoja walikubaliana kuwa wote waliohusika kuharibu miundombinu hizo za maji warejeshe kwa gharama zao haraka iwezekanavyo ili shirika liendelee kusambaza maji.

Awali mgogoro uliibuka katika kijiji hicho baada ya kuletewa mradi wa maji uliojulikana kama Olmulo development Trust (2003)ambapo wananchi hao walitakiwa kuchangia shilingi kumi(10)kwa ndoo ya maji ya lita ishirini ili kusaidia ukarabati wa mradi huo pindi miundo mbinu yake itakapoharibika ua kuchakaa huku mradi huo ukilenga kusaidia vijiji saba lakini baadhi ya wananchi wa kitongoji cha namba mbili namba tatu walikaidi hilo wakiongozwa na mzee

Aidha wakielezea madai ya kukataa kuchangia mradi huo, mzee Mesheikini alisema kuwa hawapo kuchangia mradi huo kwani awali walikuwa wakitumia maji ya mabomba yaliyowekwa na mkoloni hivyo walitaka kuendeleza mabomba hayo kwa kuyarepea tu na siyo kuweka mapya.


 

0 comments:

Post a Comment