.

.
Thursday, October 25, 2012

8:31 PM
mkuu wa mkoa akiwa na mgonjwa.JPG
mkuu wa mkoa wa Arusha alipokuwa aipokuwa akiongea na katibu wa BAKWATA mkoa wa Arusha Abubakari Jonjo katika hospitali ya mkoa Mount Meru baada ya kujeruhiwa na mlipuko

KATIKA hali isiyokuwa ya kawaida katibu wa Bakwata mkoa wa Arusha , Abdulkarimu Jonjo amenusurika kufa mara baada ya kulipukiwa na kitu kinachosadikiwa kuwa ni boma wakati akiwa amelala myumbani kwake jana majira ya saa 6;30 usiku eneo la Esso jijini Arusha.

Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kamati ya usalama inayoongozwa na mkuu wa mkoa wa Arusha Magesa  Mulongo huku akiwa amelazwa katika hospitali ya mount Meru wodi ya majeruhi, Jonjo alisema kuwa, alisema kuwa majira ya saa 6 ;30 usiku alisikia kishindo kikubwa sana dirishani kwake akiwa amelala ndipo alipoamka.

Alisema kuwa, mara baada ya kuamka aliona kitu kinachowaka kama mshumaa ambapo alijaribu kukisogelea kwa lengo la kukishika na kukichunguza ndipo ghafla kilipolipuka na na kumrusha mbali , na baada ya muda kidogo aliamka na kwenda kuomba msaada kwa majirani.

‘Kitu hicho kilinishtua sana kwani sikutarajia na mara kilipolipuka kilinisababishia nipate maumivu makali sana na mara baada ya kukaa chini kwa muda mfupi ndipo nilifaniukiwa kunyanyuka na kuomba msaada kwa majirani ambao walifanikiwa kunisaidia nna kuniwaisha hospitalini hadi mnavyoniona hapa sasa hivi , hali yangu ni nzuri na namshukuru mungu’alisema Jonjo.

Alisema kuwa, tukio hilo linamtatanisha kwani hajaweza kujua chanzo cha tukio hadi sasa hivi na anaiomba serikali iweze kufanya  uchunguzi wa haraka kwani tukio hilo linaatarisha maisha ya watu wengi kwani ni la kutisha sana .

Akingumzia tukio hilo, Mkuu wa mkoa wa Arusha mara baada ya kutembelea  hospitalini na nyumbani  kwake, alisema kuwa , tukio hilo  lina utata mkubwa na linahitaji uchunguzi mkubwa na wa haraka kwani ni tukio ambalo linasikitisha sana na limebugikwa na utata mkubwa sana.

Mulongo alisema kuwa tukio hilo linahitaji kupewa uzito mkubwa sana ndio maana askari wa jeshi la wananchi wamefika eneo la tukio ili kufanya upelelezi wa haraka na kina hivyo hatua za kinidhamu ziweze kuchukuliwa kwa haraka kwa waliohusika na tukio hilo ambalo linaatarisha maisha ya watu.

‘Ninaombeni wananchi wa Arusha wavute subiri na wasiwe na wasiwasi katika kipindi hiki ambacho tunafanya buchunguzi wa kina kuhusiana na tukio hili na ninaombeni sana lisihusishwe na maswala ni kidini , hii mapema sana kuweza kugundua chanzo cha tukio hilo na kama mtalihusisha tukio hili na maswala ya dini basi mtazua mambo mengine ambayo yatakuwa makubwa zaidi ya hayo ,hivyo naombeni mtupe nafasi tufanye uchunguzi wa kina’alisema Mulongo.

Katika hatua nyingine , Mganga mfawidhi wa hopitali ya mkoa ya Mount Meru, Dkt Ijosia Mlay alidhinitisha kupomkea katibu huyo akiwa katika hali ya maumivu sana ambapo jitihada mbalimbali za kitabibu zilifanyika ili kuweza kuokoa maisha yake  na hadi sasa anaendelea vizuri.

Alisema kuwa, katibu huyo amepata majeraha sehemu  mbalimbali za mwili wake hasa katika maeneo ya usoni, kichwani, kifuani na mkono wa kulia ambapo alikuwa akitokwa na damu usoni na kuumia mkono wa kulia.

Dkt Mlaya alisema kuwa,maumivu hayo yalitokana na kitu kinachosadikiwa na kuwa ni baruti ambayo iliwekwa mfumo wa bomu na ilipolipuka ilimsababishia  majeraha hayo na kwa sasa hivi anaendelea vizuri na ameweza kujitambua huku akiendelea  kupewa matibabu hospitalini hapo.

Hata hivyo kamanda wa polisi mkoani hapa, Liberatus Sabas amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na amesema uchunguzi unaedelea katika kuwabaini waliohusika na tukio hilo.

Awali tukio hilo limetokea siku chache tu , mara baada ya katibu huyo kutoa tamko dhidi ya vijana wanne wa dini ya kiislamu waliotekwa na watu wasijulikana na kuvuliwa nguo zote huku wakipata mateso makali sana kutokana na kile kichodaiwa kuwa vijana hao wanaunga mkono kuwepo kwa katibu huyo kuendelea kuongoza BAKWATA mkoa wa Arusha huku  kundi lingine likipinga hatua ya kuwepo kwa katibu huyo.
 

0 comments:

Post a Comment