.

.
Saturday, October 27, 2012

4:34 AM
Kamishna wa madini, Eng. Ally Samaje alipokuwa akiongea na waandishi wa habari(hawapo pichani) juu ya wizi wa madini
Wamiliki wa migodi hapa nchini wametakiwa kuwa waaminifu kwa serikali iliyowaamini  kwa kuhakikisha wanalipa kodi ili kuongeza pato la Taifa sambamba na kuisaidia serikali kupata mapato ya kuisaidia kupanga bajeti zake za maendeleo.

Rai hiyo imetolewa hivi karibuni mkoani Arusha na Kamishna wa madini hapa nchini, Eng. Ally Samaje alipokuwa akiongea na waandishi wa habari mkoani hapa.

Alisema kuwa wamiliki wa migodi kwa sasa siyo waaminifu kutekeleza masharti waliowekewa katika makubaliano ya uwekezaji katika meneo ya machimbo kwani wengi wao wamekuwa wagumu kulipa kodi kwa kuwa na visingizio visinyo na tija wala manufaa.

“Kwa sasa serikali imekuwa ikipoteza mapato mengi katika sekta ya madini kutokana na baadhi ya wamiliki wa migodi kuiibia serikali kwa kutorosha madini nje ya nchi na kukwepa kulipa kodi kwa madai kuwa hawajazalisha madini hali inayosababisha hasara kwa Taifa letu”alisema Samaje.

Aliongeza kuwa kwa sasa wanaanza mchakato mpya wa kudhibiti hali hiyo kwa kuwadhibiti wahusika wasitoroshe madini na kama watabainika basi sheria itachukua mkondo wake, ikiwemo kusitisha mkataba wa uwekezaji na machimbo hayo kurudishwa kwa serikali ya mtaa.

Aidha aliwataka Watanzania wasiwapeleke wageni migodini  kwa ajili ya kununua madini bali wathamini Rasilimali zao ikiwemo kwa kutouza madini kwa mtu (mwenyeji wala mgeni) asiye na lesseni na pia mnunuzi asikubali kununua madini bila kuwepo kwa risiti ili kuendelea kuwepo na thamani ya madini nchini kwetu badala ya madini yetu ya Tanzanite kuwa na thamani nchi za nje.

0 comments:

Post a Comment