.

.
Sunday, October 21, 2012

10:19 AM

.
Mohammed Magarief
kiongozi wa mpito wa Libya, Mohamed Magarief alipokuwa akiongea na waandishi wa habari
 
Kiongozi wa mpito wa Libya, Mohammed Magarief, amesema kuwa mwaka mmoja baada ya Kanali Gaddafi kuuwawa, nchi bado haijakombolewa kikamilifu.

Bwana Magarief - ambaye anaongoza bunge - alitoa mfano wa hali katika mji wa Bani Walid, shina la Gaddafi, ambako hivi karibuni kumetokea mapambano baina ya wapiganaji wanaounga mkono serikali na wale wanaoshukiwa kuwa wafuasi wa Gaddafi.
Bwana Magarief piya alisema kuchelewa kufanya mabadiliko ya idara ya sheria na kuunda jeshi na kikosi cha polisi rasmi, pamoja na kushindwa kuwanyang'anya silaha wapiganaji, kunazidisha wasiwasi.

chanzo cha habari BBC 

0 comments:

Post a Comment