.

.
Monday, October 22, 2012

3:32 AM
Baadhi ya wachimba migodi waliokuwa wamegoma 

Tume inayoendesha uchunguzi kuhusiana na vifo vya wachimba migodi katika machimbo ya Marikana nchini Afrika kusini, inatarajiwa kurejelea vikao vyake wakati wowote kuanzia sasa.
Vikao hivyo vilisitishwa mapema mwezi huu ili familia za wale waliofariki wakati wa vurugu za Marikana kusafiri kwenda kusikiliza vikao hivyo.
Wengi wao wanaishi mamia ya kilomita mbali na ambako tume hiyo inaendesha vikao vyake.
Mnamo mwezi Agosti Polisi iliwafyatulia risasi waandamanji katika mgodi huo na kuwaua wachimba migodi 34,baada ya vurugu kuzuka katika maandamano hayo.
chanzo cha habari : BBC

0 comments:

Post a Comment