.

.
Saturday, October 27, 2012

3:30 AM
greda likiwa kazini katika ujenzi wa  barabara ya Muriet inayojengwa kwa nguvu ya wananchi kama inavyoo okana ambapo wameomba halmashauri iwasaidie
Serikali kupitia halmashauri ya jiji la Arusha iliyoko mkoani Arusha imetakiwa kurahisisha ufikiaji wa huduma za kijamii kwa wananchi wa mtaa wa Muriet kwa kuwaunga mkono katika ujenzi waliouanza wa  barabara ya dampo yenye urefu wa kilomita sita.

mwenyekiti wa mtaa wa Muriet Francis Ndoikai Mbise alipokuwa akiomba halmashauri iwaisaidie kumalizia barabara waliyoianza

Rai hiyo imetolewa na mwenyekiti wa mtaa wa Muriet iliyoko kata ya Terrat, Francis Ndoikai Mbisse jana walipotembelewa na viongozi wa halmashauri katika eneo la ujenzi wa barabara unaoendelea ambapo alisema kuwa wamekuwa  wakiteseka sana kufikia huduma za kijamii ambazo ziko mbali na maeneo yao kutokana na ubovu wa barabara hasa mvua zikinyesha ambapo baadhi ya wagonjwa wamekuwa wakipoteza maisha njiani wakielekea kwenye vituo vya afya kutokana na kuzidiwa kabla ya kupatiwa matibabu.





“Sisi kama viongozi tuliumia na hali hiyo pindi tupatapo taarifa hizo ambapo wananchi waliamua kuchangishana fedha kwa ajili ya ujenzi wa barabara hiyo ambapo waliweza kuchanga fedha za ujenzi wa barabara hiyo kwa urefu wa kilomita 3 kwa kiwango cha changarawe lakini mahitaji yalikuwa barabara nzima yenye urefu wa kilomita sita” alisema Mbisse.





Aliongeza kuwa baada ya wananchi kuonyesha moyo wa uhitaji wa barabara kwa kuchanga fedha, ujenzi ulianza ambapo naye meneja wa eneo hili la ujenzi( site manager) Ma Jun kutoka kampuni ya Jiangxi Geo Engeneering alijitokeza kusaidia nguvu hiyo ya wananchi kwa kutoa lita 200 za mafuta ya greda, vifusi 200 vya changarawe pamoja na greda kwa ajili ya ujenzi wa bara bara hiyo iliyogharimu zaidi ya milioni 10.
Ma Jun kutoka kampuni ya Jiangxi Geo Engeneering aliyejitolea msaada kwa ajili ya kuwaunga mkono wananchi wa muriet katika  ujenzi wa barabara

“Pamoja na jitihada hizi bado hatujafikia lengo, hivyo tunaiomba halmashauri yetu itusaidie kumalizia urefu wa kilomita hizo zingine 3 zilizobaki ili kurahisisha ufuataji wa huduma za kijamii na kupunguza adha iliyopo sasa ikiwemo wanafunzi kukata tama ya kuhudhuria shule kutokana na umbali huku hakuna usafiri kutokana na ubovu wa barabara pamoja na watu kufia njiani wafuatapo huduma mbali.” Alimalizia Mbisse


0 comments:

Post a Comment