.

.
Thursday, October 25, 2012

9:33 PM
Kundi la wachunguzi wa haki za kibinadam la umoja wa mataifa limewasilisha rasmi ombi la kukutana na Rais wa Syria Basher al Assad kwa mara ya kwanza tangu Majeshi yake yaanze kupigana na wanamgambo wanaotaka kuipindua serikali yake .
Kundi hili linalongozwa na aliyekuwa kiongozi wa wapelelezi wa umoja huo, Carl del Ponte limesema lina jukumu la kushughulikia makosa mengi tu ya jinai ambayo yamefanyika .
Wakati huohuo serikali ya syria imetangaza kukubali kusitisha mapigano dhidi ya waasi kwa kipindi cha siku nne ili kuwaruhusu wasyria kuadhimisha sikukuu ya Eid ul Adha kuanzia leo siku ya ijumaa .
Awali, Habari za maafikiano ya kusitisha mapigano zilitangazwa hivi karibuni na mpatanashi wa umoja wa mataifa nchini Syria Lakhdar Brahimi.
Lakini jeshi la taifa hilo likataka kutangazwa rasmi kwa amri hiyo ya kusitishwa mapigano ikidai muda zaidi kutathmini athari kwa pande zote mbili katika mzozo huu.

0 comments:

Post a Comment