.

.
Wednesday, October 17, 2012

6:38 AM
Mjumbe wa NEC aliyechaguliwa mkoani Manyara Amani Nizar amesema kuwa baada ya kupata nafasi hiyo ya unec anaanza kwa kuwahamasisha wanachama cha chama cha mapinduzi CCM ili waweze kuelewa lengo la chama hicho katika kupambana na vitu vitatu ambavyo ni umasikini .maradhi na ujinga ambavyo vinaonekana kulalamikiwa sana na jamii kote nchini.

Nizar aliyasema hayo mwishoni mwa wiki alipokuwa akiongea na waandishi wa habari mda mchache baada ya kuchaguliwa kuwa mjume wa NEC mkoani Manyara.

Alisema kuwa suala la ajira kwa vijana bado ni changa moto kubwa kwa serikali na chama cha mapinduzi ambacho ndicho kilichopo madarakani kwa kuweka misingi mizuri inayoweza kusaidia kupunguza kero hizo kwani kupunguza au kumaliza tatizo la ajira ni njia moja kubwa inayowezesha umaskini kupungua umaskini hapa nchini
Alisema kuwa watu wanaomba kuchaguliwa lakini wanapopewa madaraka wengi  hujisahau kile walichokuwa wameahidi kwa wanachama au wananchi katika kutatua kero mbali mbali na hasa kwa vijana ambao ndiyo wapiga kura wengi kwa sasa na ndio walengwa wakubwa wa kupunguza umaskini endapo idadi yao kubwa wakiwa wana ajira ya  kujitegemea kiuchumi kuliko kuwa tegemezi.

Amani pia aliongeza kuwa yeye kama mjumbe wa nec kupitia babati vijijini yuko tayari kushirikiana na viongozi wote wa mkoa akiwemo mwenyekiti  mkoa ilikuhakikisha chama kinakuwa na mizizi imara kuanzia ngazi ya  mkoa na wilaya zake ambapo amewataka wanachama wa chama hicho kutoyumbishwa na porojo za wapinzani kwani hata wapinzani wenyewe walianza kulelewa na  CCM kwa hiyo ni vyema wakawa makini kabla ya kuchukuwa maamuzi yoyote yale
 Amesema malumbano ndani ya chama yakiwemo makundi ni moja ya sababu kubwa inayoweza kuchangia chama hicho kuangushwa iwapo makundi hayo hayatondoka na kujenga misingi ya pamoja ambapo kuongeza kuwa makundi hayo ambayo yamezuka katika matawi mengi ya chama hicho hayana sura nzuri kwa chama na jumuia zake hivyo lazima yavunjwe na wawe kitu kimoja ili kuweza kutekeleza majukumu ya kuwawakilisha watanzania kwa kutatua kero zao.

Aidha mjumbe huyo  aliyechaguliwa kwa awamu ya pili  pia aliwaasa viongozi walichaguliwa ndani ya mkoa wa manyara kufikiria ni jinsi gani watarudisha heshima ya chama hicho kutokana na wananchi wakiwemo wanachama kuanza kupoteza imani na chama hicho kutokana na utendaji mbovu wa baadhi ya watendaji walioko ndani ya chama

0 comments:

Post a Comment