WAZIRI
wa Ujenzi, Dk John Magufuli, ameanzisha operesheni maalumu ya kukamata
magari ya umma yanayotumia namba za kiraia, baada ya kubaini kuwa
yanatumika kufisidi fedha za Serikali.Waziri huyo pia ameahidi
kuwachukulia hatua kali waliouziwa magari ya Serikali na bado wanatumia
namba zile zinazoonyesha kuwa yanamilikiwa na Serikali.
Alitoa onyo hilo jijini Dar es Salaam, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari huku akiahidi kuendesha operesheni kali ya kuhakikisha wote waliokiuka taratibu wanawatiwa mbaroni. "Operesheni hii itahusisha magari yote ya Serikali Kuu, Serikali za Mitaa, Wakala wa Serikali, Mashirika ya Umma na taasisi nyingine za umma," alisema Magufuli. Alisema hivi karibuni Serikali ilibaini kuwapo kwa magari ya umma yaliyosajiliwa kwa namba za kiraia na yanatumia namba hizo kwa manufaa binafsi na hivyo kuisababishia Serikali hasara. Dk Magufuli alisema kwa kuzingatia hali hiyo, atahakikisha kuwa utaratibu wa usajili wa magari ya umma unafuatwa. “Serikali itafanya operesheni maluum ya kurejesha usajili wa magari yote ya umma kwenye utaratibu,” alisisitiza waziri huyo maarufu katika kusimamia sheria zinazohusu wizara yake. Alisema Serikali inatoa muda wa hadi kufikia Novemba 15 mwaka huu magari ya umma yenye namba za kiraia, yarejeshwe kwenye namba stahiki za magari hayo.
"Baada ya
hapo, tutatumia vyombo vya ulinzi na usalama katika kukamata magari,
pikipiki, bajaj na mitambo ya umma na tunawaomba wananchi watusaidie
kwa kutoa taarifa,"alisema Dk Magufuli.
Dk Magufuli alisema Serikali iliweka utaratibu unaozuia matumizi ya namba za kiraia kwenye magari, pikipiki, bajaj na mitambo yake na kwamba hata hivyo utaratibu huo sasa umekiukwa.
Alisema Sheria ya Usalama Barabarani ya
mwaka 1973, inaipa mamlaka, Wizara ya Ujenzi kusajili na kutunza
kumbukumbu za magari yote ya Serikali ambayo yatapewa namba
zitakazotanguliwa na JW, PT,ST, MT,CW na DFP.
Alisema magari, pikipiki, bajaj na mitambo ya umma itakayokamatwa, itapelekwa katika maeneo ya vituo vya polisi ama karakana za Tamesa mikoani na maeneo ya idara za ujenzi wilayani. Alisema wanaohusika kusimamia na kufanikisha zoezi hilo ni makatibu wakuu wa wizara zote, makatibu tawala wa mikoa yote, wakurugenzi watendaji wa halmashauri zote, watendaji wakuu wote wa taasisi na idara za serikali na watanzania wote.
Na Tausi Ally-Dar-es-salaam
|
Home
»
»Unlabelled
» WANAOFISIDI FEDHA ZA SERIKALI KWA MAGARI YA STK WASAKWA
Monday, October 22, 2012
Recent Posts
Riba kubwa na ukosefu wa elim ya biashara inafilisi wakopaji
02 February 2016Bertha Mollel0JAJI MKUU OTHUMAN CHANDE ATOA SIKU SABA KWA MAHAKIMU 508 WATOE MAELEZO KWANINI WASIFUNGULIWE MASHITAKA KWA KUFANYA KAZI CHINI YA KIWANGO
02 February 2016Bertha Mollel0WAZIRI MKUU MAJALIWA AFANYA ZIARA HOSPITALI YA RUFAA MAWENZI
02 February 2016Bertha Mollel0EALA yaombwa kuondoa Burundi katika uanachama wa jumuiya EAC
02 February 2016Bertha Mollel0
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.