.

.
Saturday, October 20, 2012

10:10 AM

Mechi kali kati ya mabingwa wa soka Tanzania bara, Simba na timu ya Ruvu shooting iliyocheza leo jijini Dar, Simba imefanikiwa kuondoka na ushindi wa mabao 3 dhidi ya wenzao ruvu waliojikakamua na mabao 2 ambapo mechi hiyo imechezwa  sambamba na mechi kati ya coast union na Mtibwa sugar mkoani Tanga ambapo Coast imewalaza wenzao Mtibwa kwa mabao 3-1.  
Kabla ya mechi hizo baadhi mabingwa wa Soka Tanzania Bara, Simba, imeondoka jijini Dar es Salaam jana kwenda Tanga tayari kwa mchezo wao wa kesho dhidi ya Mgambo JKT huku ikiwaacha mabeki wake mahiri watatu.
Hali hiyo inatabiriwa kuiweka katika mazingira magumu timu hiyo, ambayo imeshuhudiwa mara kadhaa ukuta wake ukiwa na matatizo, hasa sehemu ya kati, kabla ya hivi karibuni, Shomari Kapombe na Juma Nyoso kupunguza tatizo hilo.
Simba kesho itawakosa Kapombe anayesumbuliwa na kifundo cha mguu, Nyoso ambaye ana kadi tatu za njano na Haruna Shamte anayeuguza maumivu ya goti.
Kwa hali hiyo, Simba inatarajiwa kuwategemea mabeki wa kimataifa, Paschal Ochieng na Koman Bili Keita sehemu ya kati, ambao mashabiki wengi hawana imani nao.
Wachezaji 24 walioondoka jana mchana kwenda Tanga ni makipa Juma Kaseja, Wilbert Mweta na Waziri Ahmad, huku Mabeki ni Nassor Said Masoud ‘Chollo’, Amir Maftah, Paulo George Ngalema, Koman Bili Keita, Paschal Ochieng na Hassan Hatibu.
Viungo ni Jonas Mkude, Ramadhani Chombo ‘Redondo’, Amri Kiemba, Abdallah Seseme, Ramadhani Singano, Uhuru Selemani, Mrisho Ngassa, Mwinyi Kazimoto na Salim Kinje wakati washambuliaji ni Abdallah Juma, Daniel Akuffo, Felix Sunzu, Edward Christopher, Haruna Athumani na Emmanuel Okwi.

0 comments:

Post a Comment