.

.
Saturday, October 27, 2012

11:48 AM
 
 Rais wa Marekani Barak Obama

Zikiwa zimebaki siku kumi na moja (11) kufanyika uchaguzi wa Marekani Rais Obama ajipigia kura Chicago
Kama hatua ya kuwahimiza wafuasi wake kumpigia kura katika uchaguzi wa Novemba sita, rais wa Marekani Barack Obama ameamua kujipigia kura yake mapema katika mji wake wa nyumbani Chicago.
Na mpinzani wake Mitt Romney amejitangaza kuwa mtu wa mageuzi wakati wa kampeni katika jimbo la Ohio huku zikiwa zimesalia siku 11 kufikia uchaguzi.
Wakati huo huo rais Obama  amepata uungwaji mkono kutoka kwa Jenerali mstaafu Colin Powell ambaye ni mwanchama wa Republican mwenye siasa za wastani, wakati yeye na mpinzani wake wa chama cha Republican Mitt Romney wakiendelea na kampeni katika majimbo muhimu kujipigia debe.
Hatua ya Powell kumwidhinisha Obama ni muhimu kwa rais huyo katika juhudi zake za kutaka kuchaguliwa tena.

0 comments:

Post a Comment