.

.
Wednesday, October 24, 2012

12:14 PM
wanamgambo wa  Somalia 

Mwandishi wa habari katika jimbo lililojitenga na Somalia, Somaliland, ameuawa na watu waliokuwa wamejihami alipokuwa anarejea nyumbani kutoka kazini na kupelekea idadi ya vifo kufikia 16 kwa mwaka huu.
Ahmed Farah Ilyas alikuwa mwandishi katika eneo Las Anod, mji ambao umekumbwa na msukosuko akifanyia kazi kampuni ya Somalia ya Universal TV.
Awali
Kabla ya kuuwawa kwake, Farah alikuwa anafuatilia taarifa ya mlipuko wa mabomu ya ardhini ambayo serikali imelaumu Al Shabaab kulifanya.
Hadi sasa Ilyas ni mwandishi wa habari wa kumi na sita kuuawa nchini Somalia mwaka huu.
Tangu kuong'olewa mamlakani kwa Rais Siad Barre mwaka 1991, Somalia daima imeshuhudia wanamgambo wa Somalia wakipigania udhibiti wa Somalia.
Somaliland ilijitangazia uhuru wake baada ya kung'olewa kwa Barre na imekuwa salama ikilinganishwa na Somalia.
Eneo la Sool liko katika sehemu ambayo inadaiwa na jimbo la Puntland na imeshuhudia msukosuko siku za hivi karibuni.
Mwandishi wa BBC Hagar Jibril ambaye yuko katika eneo jirani la Burao, anasema kuwa watu walishuhudia tukio hilo wanasema Ilyas alipigwa risasi na watu wawili waliokuwa wamejihami nyakati za jioni.
Mapema siku ya Jumanne, watu wanne walijeruhiwa baada ya kulipukiwa na mabomu ya kutega ardhini ambayo gavana wa eneo la Sool Mahamed Mahamud Ali alisema yalitegwa na Al Shabaab.
Duru zinaarifu kuwa kesi dhidi ya wanamgambo hao ilianza kusikilizwa mjini Las Anod siku ya Jumanne.
chanzo cha habari: BBC

0 comments:

Post a Comment