.

.
Sunday, October 21, 2012

8:13 AM
Waziri wa nishati na madini, Prof. Sospeter Muhongo alipoluwa akiongea na waandishi na habari(hawapo pichani juu ya maazimio ya kikao juu ya maendeleo ya nchi kupitia sekta ya nishati
waandishi wa habari wakisikiliza kwa makini maazimio ya kikao cha nishati kutoka kwa waziri mwenye dhamana (hayuko pichani.

Serikali imeamua kuwasimamisha kazi kamati ya sekretariet ya nishati kwa lushindwa kufanya kazi kwa spidi italayoweza kutimiza malengo ya milenia ifikapo mwaka 2015.

Hayo yamebainishwa jijini Arusha na waziri wa nishati na madini Prof.Sospeter M. Muhongo alipokuwa akiongea na waandishi wa habari juu ya maazimio yaliyaazimia kwenye kikao cha siku tatu kilichokuwa kikijadili maswala ya maendeleo ambapo alisema kuwa wameamua kuwasimamisha sekretariet hiyo kwani wanataka kuboresha uchumi wa watanzania kupitia sekta ya nishati hivyo kamati hiyo isingeweza kuleta matokeo mazuri.

Aliongeza kuwa kwa sasa sekta ya nishati imedhamiria kukuza uchumi wa nchi kwa kuhakikisha wanazalisha umeme wa kutosha wa kutumika ndani ya nchi kwa kuwasaidia watanzania kuendesha shughuli za kimaendeleo ambapo pia kunakuwepo na umeme utakaobaki kwa ajili ya kuuza nje ya nchi  kukuza uchumi wa watanzani na Taifa kwa ujumla.

Muhongo alisema kuwa awali kulikuwepo na tatizo la umeme kutokana na kutegemea chanzo kimoja ambacho ni maji lakini sasa wanazalisha umeme kwa gesi, mafuta huku maji ikibakia nafasi ya tatu ambapo kwa sasa pia wanaanza kuzalisha umeme kwa makaa yam awe, nishati mbadala( jua, joto la ardhi na upepo)

Aidha Muhongo aliongeza kuwa kupitia mpango huo hadi kufikia mwaka 2020-2025 nchi yetu itakuwa nchi ya kipato cha kati katika nchi zinazoendelea ambapo uchumi utakuwa ambapo watanzania watakuwa wakiishi kwa dola kuanzia 4000 hadi 12500 kwa mwaka.



0 comments:

Post a Comment