Meneja
Mawasiliano wa shirika la Tanesco Bi.Badra Masoud akiongea na waandishi
wa habari juu ya mkutano wa Mawaziri wa Nishati wa Nchi za Afrika
Mashariki na Kati mwa Afrika unaotarajiwa kuanza (leo) jijini Arusha
ambapo Tanzania itakuwa mwenyeji wa mkutano huo
Tanzania imebahatika
kuwa mwenyeji wa mkutano(5) wa mawaziri wanaosimamia Nishati ya Umeme
kutoka nchi 11 zilizo Mashariki na Kati mwa Afrika wanaounda mtandao wa
nishati na umeme maarufu kama”East Afrika Power Pool (EAPP)
unaotarajiwa kuanza rasmi leo jijini Arusha
Hayo yamesemwa na
Afisa uhusiano wa shirika la umeme (TANESCO) Bi.Badra Masoud wakati
akizungumza na waandishi wa habari juu ya mkutano huo mkubwa ambao
unatarajiwa kufanyika jijini hapa
Bi.Masoud alisema
kuwa Tanzania ni mwanachama wa mtandao wa (EAPP) ulionzishwa miaka 6
iliyopita ikiwa na lengo la kurahisisha upitakanaji wa nishati ya
uhakika ya umeme kwa nchi wanachama wa EAPP kwa kujenga njia kuu ya
kusafirishia umeme unaounganisha nchi hizi.
Alifafanua kuwa
Tanzania inahitaji kuboresha maisha ya wananchi wake katika Nyanja
nyingi kama vile matibabu,elimu,upatikanaji wa maji safi na
salama,uzalishaji,Ongezeka la viwanda na kurahisisha matumizi ya
majumbani.
Alisema
kuwa haya yote yatawezekana tu kama kutakuwa na umeme wa uhakika na
wenye gharama nafuu ili wananchi waweze kumudu gharama hizo bila
matatizo yeyote.
Bi.Masoud alisema
ili kupata umeme wa uhakika na gharama nafuu,Mawaziri wa nchi hizi 11
watatoka na mwongozo wa utekelezaji wa kuunganisha miundombinu ya njia
kuu ya kusafirisha umeme kwenye nchi za Afrika Mashariki na Kati mwa
Afrika.
“kwa sasa tunanunua
umeme bei ghali sana kutoka kwa wazalishaji binafsi (Independent Power
Producer-IPP) ambao wanatuuzia umeme kwa bei ghali sana hivyo TANESCO
inaponunua umeme kwa bei ghali sana na kuiuza kwa bei kawaida
inaipelekea kupata hasara na hata kupandisha bei ili kukidhi gharama za
uendeshaji.”alisema Badra
Wanahabari wakiwa kazini
Hata hivyo alisema
kuwa mkutano huo utatanguliwa na Wakurugenzi wa mashirika yaliyo na
dhamana ya kuzalisha,kusafirisha na kusambaza umeme,wakiwepo wadau wa
Mamlaka za Udhibiti wa Nishati ya Umeme wataanza mkutano wa awali
utakaofuatiwa na mkutano wa Mawaziri siku ya Jumamosi.
Alisema kuwa nchi
wanachama wa EAPP,ni Tanzania
,Kenya,Uganda,Ethiopia,Rwanda,Burundi,Libya,Egypt,Republic of
Sudan,Demokratic Republic of Congo(DRC) na Djbouti.
0 comments:
Post a Comment