mkuu wa mkoa wa Arusha alipokuwa aipokuwa akiongea na katibu wa BAKWATA mkoa wa Arusha Abubakari Jonjo katika hospitali ya mkoa Mount Meru baada ya kujeruhiwa na mlipuko
KATIKA hali isiyokuwa ya kawaida katibu wa Bakwata mkoa wa
Arusha , Abdulkarimu Jonjo amenusurika kufa mara baada ya kulipukiwa na kitu
kinachosadikiwa kuwa ni boma wakati akiwa amelala myumbani kwake jana majira ya
saa 6;30 usiku eneo la Esso jijini Arusha.
Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kamati ya
usalama inayoongozwa na mkuu wa mkoa wa Arusha Magesa Mulongo huku akiwa amelazwa katika hospitali
ya mount Meru wodi ya majeruhi, Jonjo alisema kuwa, alisema kuwa majira ya saa
6 ;30 usiku alisikia kishindo kikubwa sana
dirishani kwake akiwa amelala ndipo alipoamka.
Alisema kuwa, mara baada ya kuamka aliona kitu kinachowaka
kama mshumaa ambapo alijaribu kukisogelea kwa lengo la kukishika na
kukichunguza ndipo ghafla kilipolipuka na na kumrusha mbali , na baada ya muda
kidogo aliamka na kwenda kuomba msaada kwa majirani.
‘Kitu hicho kilinishtua sana kwani sikutarajia na mara
kilipolipuka kilinisababishia nipate maumivu makali sana na mara baada ya kukaa
chini kwa muda mfupi ndipo nilifaniukiwa kunyanyuka na kuomba msaada kwa
majirani ambao walifanikiwa kunisaidia nna kuniwaisha hospitalini hadi
mnavyoniona hapa sasa hivi , hali yangu ni nzuri na namshukuru mungu’alisema
Jonjo.
Alisema kuwa, tukio hilo
linamtatanisha kwani hajaweza kujua chanzo cha tukio hadi sasa hivi na anaiomba
serikali iweze kufanya uchunguzi wa
haraka kwani tukio hilo linaatarisha maisha ya
watu wengi kwani ni la kutisha sana
.
Akingumzia tukio hilo, Mkuu wa mkoa wa Arusha mara baada ya
kutembelea hospitalini na nyumbani kwake, alisema kuwa , tukio hilo lina utata mkubwa na linahitaji uchunguzi
mkubwa na wa haraka kwani ni tukio ambalo linasikitisha sana na limebugikwa na
utata mkubwa sana.
Mulongo alisema kuwa tukio hilo linahitaji kupewa uzito
mkubwa sana ndio maana askari wa jeshi la wananchi wamefika eneo la tukio ili
kufanya upelelezi wa haraka na kina hivyo hatua za kinidhamu ziweze kuchukuliwa
kwa haraka kwa waliohusika na tukio hilo ambalo linaatarisha maisha ya watu.
‘Ninaombeni wananchi wa Arusha wavute subiri na wasiwe na
wasiwasi katika kipindi hiki ambacho tunafanya buchunguzi wa kina kuhusiana na
tukio hili na ninaombeni sana lisihusishwe na maswala ni kidini , hii mapema
sana kuweza kugundua chanzo cha tukio hilo na kama mtalihusisha tukio hili na
maswala ya dini basi mtazua mambo mengine ambayo yatakuwa makubwa zaidi ya hayo
,hivyo naombeni mtupe nafasi tufanye uchunguzi wa kina’alisema Mulongo.
Katika hatua nyingine , Mganga mfawidhi wa hopitali ya mkoa
ya Mount Meru, Dkt Ijosia Mlay alidhinitisha kupomkea katibu huyo akiwa katika
hali ya maumivu sana
ambapo jitihada mbalimbali za kitabibu zilifanyika ili kuweza kuokoa maisha
yake na hadi sasa anaendelea vizuri.
Alisema kuwa, katibu huyo amepata majeraha sehemu mbalimbali za mwili wake hasa katika maeneo
ya usoni, kichwani, kifuani na mkono wa kulia ambapo alikuwa akitokwa na damu
usoni na kuumia mkono wa kulia.
Dkt Mlaya alisema kuwa,maumivu hayo yalitokana na kitu
kinachosadikiwa na kuwa ni baruti ambayo iliwekwa mfumo wa bomu na ilipolipuka
ilimsababishia majeraha hayo na kwa sasa
hivi anaendelea vizuri na ameweza kujitambua huku akiendelea kupewa matibabu hospitalini hapo.
Hata hivyo kamanda wa polisi mkoani hapa, Liberatus Sabas
amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na amesema
uchunguzi unaedelea katika kuwabaini waliohusika na tukio hilo.
Awali tukio hilo limetokea siku chache tu , mara baada ya
katibu huyo kutoa tamko dhidi ya vijana wanne wa dini ya kiislamu waliotekwa na
watu wasijulikana na kuvuliwa nguo zote huku wakipata mateso makali sana
kutokana na kile kichodaiwa kuwa vijana hao wanaunga mkono kuwepo kwa katibu
huyo kuendelea kuongoza BAKWATA mkoa wa Arusha huku kundi lingine likipinga hatua ya kuwepo kwa
katibu huyo.
|
Home
»
»Unlabelled
» KATIBU WA BAKWATA MKOA WA ARUSHA ANUSURURIKA KUFA
Thursday, October 25, 2012
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment