WENYEJI
wa michuano ya Mataifa ya Afrika 2013, Afrika Kusini itakata utepe wa
michuano hiyo kwa kucheza na Cape Verde ambao waliwashangaza mabingwa wa
zamani wa Afrika Cameroon na kukata tiketi ya kushiriki michuano hiyo
kwa mara ya kwanza. Morocco ambao watakuwa wenyeji wa michuano hiyo
mwaka 2015 sambamba na Angola ndio wanakamilisha timu za kundi A.
Mabingwa watetezi wa michuano hiyo Zambia wamepangwa kundi moja na
Nigeria pamoja na Ethiopia na Burkina Faso katika kundi C huku kundi B
likiwa na timu za Ghana, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Niger na
Mali. Katika Kundi D ambalo wadau wengi wa mchezo wa soka wanasema ndio
kundi la kifo lina timu za Ivory Coast, Togo, Tunisia na Algeria ambapo
michuano hiyo inatarajiwa kuanza kutimua vumbi Januari 19 mpaka Februari
10 mwakani.
Home
»
»Unlabelled
» IVORY COAST, TOGO, TUNISIA, ALGERIA KUNDI LA KIFO AFCON 2013.
Thursday, October 25, 2012
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment