Takriban
watu saba wameuawa nchini Nigeria na wengine wengi wakijeruhiwa katika
shambulio la kujitoa mhanga katika kanisa la kikatoliki Kaskazini mwa
Nigeria.
Maafisa wanasema kuwa gari
lililokuwa limebeba mabomu liliingia katika kanisa hilo na kulipua
mabomu huku athari zake zikitoboa shimo katika paa la kanisa hilo.
Aidha Shambulio
hilo lilitokea mjini Kaduna, eneo ambalo limekuwa likilengwa sana na
wapiganaji wa Boko Haram kwa mashambulizi katika siku za hivi karibuni.
Rais
Goodluck Jonathan ameahidi kongeza juhudi za kupambana na ugaidi na
vurugu nchini humo.
Aidha Rais Goodluck alitaja shambulizi hilo kama
kitu kisicho kubalika na ambacho kinatishia usalama na uthabiti wa nchi
hiyo.
Mwandishi wa BBC mjini huko anaarifu
kuwa shambulio hilo lilitokana na bomu lilotegwa kwenye gari
lililopuliwa na mtu aliyejitoa mhanga na kugonga gari hilo kwenye ukuta
wa kanisa.
Anasema uharibifu mkubwa ulitokea ndani ya jengo na kwamba mapaa ya maduka na nyumba za karibu yaling'oka.
Afisaa wa kanisa alisema watu kama wanne waliuwawa na wengine wengi kujeruhiwa.
Wakuu
wanasema vijana wa Kikristo walioingiwa na hasira kwa sababu ya tukio
hilo, walishambulia gari la serikali ambalo lilikwenda kusaidia
manusura.
Kumetokea mashambulio kadha ya kidini katika jimbo hilo, mengi yamefanywa na kundi la wapiganaji wa kiislamu, Boko Haram
chanzo cha habari:BBC
0 comments:
Post a Comment