vijana walioudhuria semina ya uraia na kutoa maoni ya katiba mpya inayotarajiwa kwenda kwa mkuu wa wilaya ya Arusha hivi karibuni ili kujihami endapo tume haitawapitia basi maoni yao yasibaki bali yawasilishwe na mkuu huyo
Imeelezwa kuwa uongozi usio
na tija ni mzigo kwa watanzania ambao ni walipa kodi hivyo katiba ijayo
ielekeze wizara zilizopo ili kuweka ukomo wa wiraza zinazoibuliwa kila siku
bila tija wala manufaa kwa watanzania.
Hayo yamezungumzwa mkoani na
Arusha na vijana wa kata ya daraja mbili na Lemara kwenye semina ya siku tatu
ya Uraia iliyoandaliwa na Asasi isiyo ya kiserikali iitwayo Mategemeo Women
Association(MWOA) na kuwezeshwa na Foundation for civil society.
Semina hiyo iliyowapatia
vijana hao elimu ya uraia, wajibu na haki pamoja elimu ya katiba kwa ajili ya
kujua kazi zake pamoja na katiba iliyopo kwa ajili ya kutoa maoni yao walipewa
nafasi ya kutoa maoni yao ambapo walisema kuwa kuwepo kwa wizara nyingi
serikalini ni mzigo usio na tija kwa walipa kodi(Watanzania).
Waliongeza kuwa kutokana na
hayo wanaomba katiba ijayo ipunguze mzigo huo kwa kuweka ukomo wa wizara
serikalini zinazojulikana tena zenye tija kwa watanzania na taifa kwa ujumla
kuliko kila kiongozi akiingia madarakani kubuni wizara yake na kuweka watu wake
hata wasio na sifa wala taaluma.
Mbali na hilo Waliongeza kuwa katiba ijayo iweke wazi
madaraka ya viongozi wetu kwa kutoruhusu mtu mmoja kushika nyadhfa nyingi kwa
wakati mmoja ikiwemo mbunge kutoruhusiwa kuwa waziri kwani kufanya hivyo ni
kuwanyima watanzania wengine nafasi za ajira na kuwanyima haki wananchi
waliomchagua kuwawakilisha(kuwasemea bungeni) badala yake anakuwa anaisemea
serikali na kuwasahau wananchi.
Aidha katiba ijayo piaielekeze namna ya kumuondoa madarakani kiongozi
anayechaguliwa na wananchi anaposhindwa kazi ya kiutekelezaji na kuwa kiongozi
mbovu kwa kuhamasisha maswala ya rushwa, uvunjifu wa amani, uhalifu n.k na
kumchagua mwingine ili kuwaondoa viongozi watakaokuwa wabadhirifu wa fedha za
umma na wazembe katika kuwatumikia wananchi.
Mmoja wa vijana hao Ally
Manyanya alisema kuwa pia Rais apunguziwe madaraka ikiwemo uteuzi wa baadhi ya
watendaji wa umma kama TAKUKURU na tume ya uchaguzi kwani hujikuta wakifanya
kazi chini ya rais na chama chake hivyo wamependekeza kuwa watendaji hao
wapitishwe na bunge sambamba na Rais kuteua mawaziri kulingana na taaluma zao
ili kutenda kazi kwa ufanisi zaidi.
Manyanya aliongeza kuwa mbali
na hayo pia katiba ijayo iamue na kuelekeza au kufafanua muundo wa serikali ya
muungano kwani kwa sasa Tanganyika Tunajiita Wanzania huku Wazanzibar wakibaki
na jina lao na kuwa na serikali yao, katiba na bunge hivyo katiba ielekeze
muungano huu kama muungano kuwe na serikali moja ua Tanganyika wawe na serikali
yao na Zanzibar serikali yao huku wakiwa chini ya serikali nyingine ya tatu ya
Jamhuri.
Kwa upande wake Shaban
Willium alipendekeza katiba ijayo iondoe kikwazo cha ajira kwa vijana ikiwemo
kuajiriwa bila kuzingatiwa uzoefu wake bali taaluma yake, piaviongozi wa serikali kuanzia ngazi za chini
akiwemo balozi wa nyumba kumi, mwenyekiti n.k walipwe posho ili kupunguza
upmbaji na upokeaji wa rushwa kwao pia uongozi wa balozi usitokane na chama
tawala bali mfumo wa vyama vingi kama mwenyekiti.
Aliongeza kuwa katiba ijayo
pia ieleze mfumo maalum wa elim kuliko kila kiongozi kuingia na mfumo wake pia
Mila, Tamaduni na Desturi ziwe na mipaka ya kutovunja sheria za nchi kwa kigezo
cha mila, desturi na utamaduni, ambapo pia alipendekeza adhabu ya kifo kuondolewa
kwani adhabu hiyo inakiuka haki za binadamu ya “kila mtu ana haki yan kuishi”.
Naye mwenyekiti wa Asasi hiyo
ya MWOA, Bi, Agness Saibulu alisema kuwa semina hiyo ya siku tatu
iliyowashirikisha vijana 30 kutoka katika mitaa ya kata za daraja mbili na
lemera wamefanikiwa kujifunza historia fupi ya Tanzaniia, elimu ya uraia, haki
na wajibu wa kijana katika kushiriki mambo ya maendeleo ikiwemo vikao vya
kiserikali, upigaji kura n.k pamoja na katiba, demokrasia, uongozi na uchumi
ambapo pia wametoa maoni yao ya katiba mpya na kuipeleka kwa mkuu wa wilaya
kuiwasilisha endapo tume haitawafikia.
kushoto ni mratibu wa semina hiyo ya uraia, Violla Ndikindikoki akiwa na mwenyekiti wa Asasi ya MWOA, Agness Saibulu (wa katikati), anayefuata ni mmoja wa wakufunzi wa semina hiyo Isaya Doita(kulia) ambaye pia ni diwani wa kata ya ngarenaro jijini Arusha wakijadiliana jambo.
0 comments:
Post a Comment