.

.
Wednesday, October 24, 2012

9:18 PM
Polisi wakionekena wakimshambulia aliyekuwa mwandishi wa habari Daudi mwangosi na kupelekea kifo chake huko Nyololo, Mufindi, lakini anayesomewa shtaka leo ni mmoja tena asiyefehemika kutokana na kufichwa na jeshi hilo.

JESHI la Polisi mkoani Iringa, limeendeleza usiri mkubwa wa kumficha mtuhumiwa wa mauaji ya aliyekuwa mwandishi wa habari wa kituo cha runinga cha Channel Ten, Daudi Mwangosi.
Ikiwa ni mara ya tatu kwa mtuhumiwa huyo, Pasificus Cleophace Simon (23), kufikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi jana, ulinzi mkali ulitawala eneo hilo, huku waandishi wakipigwa vikumbo wakizuiwa kupiga picha.
Askari wenye sare wa Kikosi cha Kuzuia Ghasia (FFU) wakiwa na virungu, silaha za moto huku wengine wakivalia kiraia, walitanda mahakamani hapo kuhakikisha hakuna mwandishi anampiga picha mtuhumiwa huyo.
Katika patashika hiyo, mwandishi wa habari wa gazeti la Majira, Eliasa Ally, alijikuta akipigwa na askari ambao walikuwa wakimzuia kupiga picha.
Askari aliyempiga mwandishi huyo alitambulika kwa jina moja la Idirisa, na hivyo tukio hilo likazidisha uhasama baina ya jeshi hilo mkoani hapa na waandishi wa habari.
Mtuhumiwa huyo alifikishwa mahakamani akiwa amevalia jaketi lenye kofia iliyomfunika kichwa kizima kiasi cha sura yake kutotambulika.
Akiwa mahakamani hapo, wakili wa serikali ambaye pia ni mwendesha mashtaka ya mtuhumiwa huyo, Lilian Ngilangwa, alimweleza Hakimu Mkazi Mwandamizi, Dyness Lyimo, kuwa upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika.
Lyimo aliomba kesi hiyo ihairishwe hadi Novemba 7 mwaka huu itakapotajwa tena.
Pasificus alifikishwa mahakamani hapo, akidaiwa kumuua kwa makusudi Mwangosi wakati wa ufunguzi wa matawi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) katika Kijiji cha Nyololo, Wilaya ya Mufindi, Mkoa wa Iringa, mnamo Septemba 2, mwaka huu.

0 comments:

Post a Comment