Asha Maulid,
Msichana mwenye umri wa miaka 20 na mkazi wa Kijiji cha Nduruma Wilaya ya
Arumeru, anamlalamikia askari polisi mmoja, aliyefahamika kwa jina la Saidy
Rashidi wa Kituo Kikuu cha Polisi Jijini kwa kumtelekeza baada ya
kumzalisha.
Akizungumza
Kituoni hapo Alhamis iliyopita, Asha aliwaambia Wandishi wa habari kwamba,
alizaa na askari huyo mtoto wa kiume aitwaye Nasri Saidy ambaye sasa ana umri wa
miezi nane baada ya kuishi kama wapenzi na askari huyo katika
makazi ya askari jijini hapa.
Msichana huyo
aliendelea kudai mbele ya Wandishi wa Habari waliokuwa wamekusanyika ofisini kwa
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha kufuatilia habari za kipolisi kwamba alitokea
kupendana na askari huyo hatimaye kuishi naye katika nyumba za askari zilizoko
maeneo ya kituo kikuu cha polisi ambapo baada ya miezi kadhaa askari huyo
alimlazimisha kumzalia mtoto bila kufunga naye ndoandoa.
“Baada ya
miezi kadhaa ya kuishi naye akawa ananilazimisha kumzalia mtoto bila ndoa ambapo
nikimuuliza alikuwa anasema kwa kuwa ananipenda hakuna shida tutaoana baada ya
kuruhusiwa kuoa na mwajiri wake, kwani kwa sasa hawaruhusiwi kuoa kutokana na
cheo chake, hivyo baada ya kuona kero za kuzaa zinazidi niliamua kubeba mimba
ambapo ndipo hapo matatizo yalipoanzia”, alisema Asha.
Aliongeza:
“Baada ya kubeba mimba na kufikia miezi 8 mwanaume akawa ananinyanyasa na
kunipiga kila siku hadi kutokwa damu puani hali iliyonisababisha
kumwambia naenda kwetu”, alilalamika Asha na kuongeza:
“Baada
aliniambia nichukue kila ninachoweza kuchukua na baada kuchukua alikuja nyumbani
kwetu wakati sipo na kuvichukua na kwenda polisi kuandika maelezo kuwa mimi
nimemvunjia nyumba na kumwibia vitu”, alidai Asha.
Asha alidai
kwamba hali hiyo ilimsababishia wazazi wake kumchukia kutokana na askari huyo
kuwadharau na kutumia uaskari wake kuwatishia ndugu zangu kuwa atawashtaki hali
iliyowafanya ndugu hao kukosa amani.
Anasema
kutokana na wazazi wake na ndugu wengine kumchukia alilazimika kuomba hifadhi
kwa mama yake mdogo:
“Huko
nilidhani nitapata ahueni kutokana na manyanyaso yake lakini huko ndiko nimekuwa
nikiambulia kipigo kutoka kwa mwaname huyu na hatimaye kusababisha mama mdogo
naye kunifukuza”, alieleza Asha kwa masikitiko huku akiwa amembeba mtoto wake
Nasri ambaye alionekana na kuwa na siha njema na mchangamfu wakati
wote.
Asha
aliendelea kusema kuwa awali baada ya askari huyo kumfukuza nyumbani kwake
alikuwa akimfuata siku moja moja kumtaka mumewe huyo kumpatia fedha za matumizi
ya mtoto lakini alikuwa anaambulia matusi na kejeli kutoka kwa mumewe na pia
wenzake walikuwa wakimshinikiza kumuweka ndani ya mahabusu ambapo aliwahi
kulazwa kituoni hapo bila kosa wala maelezo kwa madai kuwa amekuwa
msumbufu.
Aidha alidai
kuwa kutokana na mpenzi wake huyo kukataa kutoa fedha za malezi ya mtoto wao,
aliamua kwenda kumshitaki Idara ya Ustawi wa Jamii, ambako anasema walimpa barua
ya kumpelekea Mkuu wa Polisi Kituo cha Kikuu (OCS).
“OCS
alimwita mzazi mwenzangu huyo na kumkabidhi barua hiyo ya Ustawi
wa Jamii ambapo aliahidi kutoa matumizi ya mtoto lakini hadi sasa
hakuna chochote anachotoa kwa ajili ya mtoto ambapo na zaidi ya hayo mwanzoni
mwa Oktoba alikana kumtambua huyu mtoto wala na hata mimi mama yake”,
alilalamika Asha kwa uchungu mkubwa.
Asha anasema
kutokana na hali hiyo, naliomba Jeshi la Polisi kumsaidia kumsimamia askari huyo
(mumewe) ili mtoto wake apate matunzo mazuri kwani ni haki ya mtoto huyo nay eye
kupata matunzo kutoka kwa askari huyo.
Gazeti hili
lilipowasiliana na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Arusha Liberatus Sabas,
kuhusiana na madai ya msichana huyo, Kamanda huyo alitoa kauli tata.
Kwanza
alisema azingeweza kuzungumzia suala hilo kwa madai kwamba hayo ni mambo binafsi
lakini pia akasema kwamba kwa kuwa malalamiko hayo yanamhusisha askari wake
atayafuatilia.
Kauli hizo
tata za Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Arusha zinafanya madai ya awali
yaliyotolewa na Asha kwamba askari huyo amekuwa akitumia kivuli cha Jeshi la
Polisi kumnyanyasa nay eye, mtoto wake, wazazi wake na familia yake kwa ujumla
kuwa yanaweza kua na ukweli ndani yake.
0 comments:
Post a Comment