Kulia
Mjumbe wa Kamati kuu ya chama cha mapinduzi Goodfrey Mwalusamba (MNEC)
akimnadi mgombea udiwani kata ya daraja mbili Philip Mushi Philip
katika kampeni za uchaguzi mdogo
Kampeni
za uchaguzi mdogo katika kata ya daraja mbili jijini Arusha zimeendelea
kupamba moto huku kila aina ya vituko vikigubika chaguzi hizo ambapo
Chama cha mapinduzi CCM kimetamba kuibuka kidedea katika uchaguzi huo
mdogo wa udiwani katika kata ya daraja mbili jijini Arusha
|
Wananchi wa kata ya daraja mbili wakiwa makini katika kusikiliza sera za CCM. |
Pia
chama hicho kimerushia kombora kwa chama cha demokrasia na maendelo
chadema kwa kusema kuwa watalinda kura kwa bastola huku wakishindwa
kutumia majukwaa vizuri badala yake chama hicho kimekuwa kikitumia
nafasi hiyo kutukana majukwaani
Akimnadi
mgombea udiwani kata ya daraja mbili Mjumbe wa Kamati kuu ya chama cha
mapinduzi Goodfrey Mwalusamba alisema bila kutaja jina la chama kuwa
haina sera zaidi ya vitisho,matusi sanjari na vituko vya kila aina
kwa madai kuwa watalinda kura kwa bastola
“Utaskia
wanasema kuwa tuna Mungu huku wakidai watalinda kura na bastola ,,ndani
ya CCM hakuna wanafki,wazushi watuonyeshe ni mangapi waliyoyafanya hadi
sasa”alisema Mwalusamba
Kikundi cha masanja kikicheza ngoma
Aliongeza
kuwa Nchi inaongozwa kwa misingi ya haki na sio vinginevyo huku
akiwatahazarisha vijana kutokufata mikumbo ya hapa na pale na
kunyweshwa pombea aina ya viroba ili wawatukane CCM huku akiwasihi watu
kumpa kura Philip mushi ili kuharakisha maendeleo ya kata hiyo kwa kuwa
wapinzani hao hawamtambui Meya wa jiji la Arusha
Naye
mgombea wa udiwani Philip Mushi Philip alisema kuwa endapo watampa
ridhaa ya kuongoza kata hiyo ni wazi kuwa atashughulikia mambo
yafuatayo ikiwa ni ,kuboresha zahanati,barabara,mikopo kwa akina mama
pamoja na vijana kujikita katika ujasiriamali
0 comments:
Post a Comment