BAADHI ya wananchi wa Zanzibar, wamelalamikia kile
walichokielezea kuwa ni ukiukwaji wa haki za binadamu, unaofanywa na
polisi katika operesheni ya kuwasaka wahalifu na watu wanaotuhumiwa
kuchochea vurugu visiwani humu.
Operesheni
hiyo inafuatia matukio ya uvunjifu wa amani ulioambatana na uharibifu
wa mali hasa baada madai ya kutoweka ghafla kwa Kiongozi wa Taasisi za
Kiislamu, Sheikh Farid Hadi Ahmed, Oktoba 16 mwaka huu.
Jana
zaidi ya watu 50 walikutana na waandishi wa habari na kulalamikia
vitendo vya ukiukwaji wa haki za binadamu katika operesheni ya kuwasaka
watuhumiwa.
Kwa
mujibu wa watu, kijana mmoja aliyetambuliwa kuwa ni Hamad Ali Kaimu,
amekufa baada ya kupigwa na askari wa vikosi vya usalama katika
operesheni hiyo.
Miongoni
mwa waliozungumza na waandishi ni, baba mzazi wa kijana huyo, Ali Kaimu
mkazi wa eneo la Nyerere, ambaye alidai kuwa mtoto wake alipigwa hadi
kufa akiwa mikononi mwa polisi na kwamba tukio hilo lilitokea Oktoba
27, mwaka huu.
Kaimu alisema kitendo hicho hakikubaliki na kwamba hatua lazima zichukuliwe dhidi ya wahusika.
Baba
huyo wa marehemu, alisema alimuona mtoto wake akiitwa na polisi wakati
akienda kuchunga ng’ombe na kwamba baadaye askari walianza kumpiga
kijana huyo akiwa mbele ya macho yake.
“Mwanangu
aliniita baba njoo uchukue mzigo wangu na nikuonyeshe nilipomfunga
ng’ombe wangu na nilipokwenda polisi na mie wakaniangushia kipigo
kikali sana. Mwanangu alikuwa na Sh50,000 za kununulia godoro na
alitaka kunipa lakini walikataa asinikabidhi” alisema baba huyo kwa
huzuni.
Alisema kijana wake alikamatwa na siku ya Sikukuu ya Idd El Hajj na wakati akichunga ng’ombe huko Magomeni.
Kaimu
alisema siku ya pili alipigiwa simu akiitwa katika katika Kituo cha
Polisi cha Madema na alipokwenda alitakiwa kwenda katika Hospitali ya
Mnazi Mmoja kuchukua mwili wa mtoto wake.
“Walinipigia
simu nikachukue maiti yangu na mimi nikagoma kwa sababu wamemchukua
mwanangu akiwa hai na nikawaambia munikabidhi mwanagu akiwa hai vipi
watanipa mwanangu maiti,” alihoji mzee huyo.
0 comments:
Post a Comment