baadhi ya wanawake walioandamana hadi ofisi za mkuuwa wilaya ya Arusha John Mongeal kuwasilisha kilio chao cha uhba wa maji. |
Wanawake zaidi ya 500 kutoka katika kata ya Terrat iliyoko jijini Arusha wameandamana mapema jana hadi kwenye ofisi za mkuu wa wilaya ya Arusha John Mongela wakiwa na kilio kikubwa juu ya swala la maji ambalo imekuwa kama Almasi katika kata hiyo.
Wananchi hao waliosikilizwa na katibu tawala wa Mkoa wa Arusha, Sanford Yakobo Shayo, walisema kuwa wamekuwa na Tatizo la maji tangu mwaka huu uanze hawajapata maji katika kata yao hali iliyowalazimu kutembea umbali mrefu kufuata huduma hiyo ambao mwanzo wa kiangazi hiki walichangishwa fedha shilingi 10000 kila mwananchi na kupatikana fedha zaidi ya 3 lengo likiwa la kuunga maji lakini hadi leo hakuna mafanikio huku viongozi wakiwa kimya juu ya hilo
Mmoja wa wananchi hao Nganashe Lestoni alisema mbele ya mkuu huyo kuwa waathirika wakubwa wa tatizo hilo la maji ni wanawake na watoto kwani hulazimika kuamka saa tisa za usiku kwenda kutafuta maji ambapo huacha watoto wakiwa wamelala na kurudi saa saba mchana na kukuta watoto wao wameteseka na njaa.
Aliongeza kuwa mbali na kuteseka na baridi na hofu ya hatari za barabarani ikiwemo wanyama wakali, wamekuwa wakipigwa na waume zao wakichelewa kurudi kwa madai kuwa walikuwa kwa wanaume wengine hali ambayo si ya kweli bali ni mfumo dume uliopo kwenye kabila hilo la kimaasai.
Wananchi hao wamewashutumu viongozi wao kuanzia ngazi za vijiji akiwemo diwani wa kata hiyo kwa kuendekeza mabishano ya kisiasa na kushindwa kushughulikia swala hilo kwani liko ndani ya uwezo wake badala yake wananyamazia kero hizo kukomoana kwa maslahi yao binafsi bila kujali wananchi ndio wanaumia.
Kwa upande wake katibu huyo wa mkoa Shayo aliwataka wananchi hao kurudi makwao na swala lao linaanza kufanyiwa kazi ambapo aliteua kamati maalum hapo hapo ya kufuatilia swala hilo ambao ni miongoni mwa wanawake hao.
Katibu tawala wa mkoa, Yakobo Shayo na kushoto(mwenye suti ya rangi ya udongo) akiwa na kamata ya maji aliyoiteua na mwenye suti nyeupe kushoto ni mkuu wa upelezi mkoa Arusha kamanda Mvula. |
0 comments:
Post a Comment