Watoto watano ,watatu wakiwa wa familia moja wamekufa Wilayani Karagwe mkoani Kagera.
Ni
baada ya kulipukiwa na bomu la kutupwa kwa mkono wakati walipokuwa
wakichezea Bomu hilo lililookotwa kwenye vyuma chakavu na kudhani kuwa
ni mpira.
Tukio
hilo lilitokea Juma tano majira ya asubuhi huko Wilayani Karagwe mkoani
Kagera Magharibi mwa Tanzania wakati watoto walipokuwa wakichezea kitu
mfano wa mpira mdogo ,ambacho baadaye kilikuja kutambulika kuwa
lilikuwa Bomu la kurushwa kwa mkono.
Mkuu wa Wilaya wa Karagwe Bi Darli Rwegasira amesema kuwa watoto hao
walilipukiwa na Bomu hilo ambapo watatu kati yao walikufa papo hapo
huku wawili wakifia hospitalini.
Kwa
Mujibu wa Mkuu huyo wa Wilaya, awali mzazi wa watoto hao amekiri kuwa
aliliona bomu nyumbani kwake hapo juzi ambapo watoto wake walikuja nalo
baada ya kuliokota huku wakidhani kuwa ni mpira.
Naye
Kamanda wa Polisi mkoani Kagera Philipo Kalangi alisema kuwa utafiti
waliofanya umeonyesha kuwa Bomu hilo lililookotwa na kijana mmoja
ambaye alikuwa akikusanya vyuma chakavu kwa lengo la kuviuza hapo
wilayani karagwe.
Bomu hilo lilikuwa
mojawapo katika vyuma alivyokuwa ameokota na baadaye watoto hao
walienda kulichezea nyumbani kwao na hatimaye kusababisha maafa hayo.
Mkuu
huyo wa Polisi mkoani Kagera alidokeza kuwa uchunguzi unaendelea ili
kujua kwa undani Bomu hilo lilitokea wapi na iwapo kama kuna mabomu
mengine yanayoweza kuwa yamebaki katika maeneo mbali mbali hapo
Wilayani Karagwe.
Mkuu huyo wa Polisi
hakuweza kukiri wala kukana moja kwa moja kuhusisha Bomu hilo Kama
matokeo ya uwepo wa wakimbizi wa Rwanda waliowahi kuishi Wilayani hapo
mwaka 1994 baada ya mauaji ya kimbari nchini Rwanda ambapo Wilaya ya
Karagwe ni moja ya wilaya zilizopokea wakimbizi wengi kutoka nchini
Rwanda.
Uchunguzi zaidi unaendelea huku ukiwahusisha wataalam wa milipuko kutoka Polisi na jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania.
0 comments:
Post a Comment