mwanafunzi wa shule ya Kinyaki aliyekamtwa kwa amri ya mkuu wa mkoa, baada ya kuandanama kushinikza mwalimu mkuu kuondolewa shuleni kwao |
MKUU wa Mkoa wa Arusha Magesa Mulongo amewasweka rumande wanafunzi watatu
wa Shule ya Sekondari Kimnyaki kwa kutoridhishwa na maelezo ya sababu za maandamano yao na wanafunzi wenzake hadi Ofisini kwake.
Wanafunzi hao waliokamatwa wakati wakijieleza kusudio la maandamano yao ni pamoja na Ezekiel Memiri, Losijaki Lunde, na
Meshack Lomnyaki ambapo walisema kuwa wamekuwa wakinyanyaswa na walimu wao
shuleni ikiwemo kuwafanyisha kazi za nyumbani kama
ma-house girl.
Maandamano ya wanafunzi hao yalikuwa na lengo la kushinikiza Mkuu wao wa
shule ya kinyaki mwalimu Mariam Chamle kuondolewa kwa kuwa chanzo cha matatizo
shuleni hapo ikiwemo kushusha kiwango cha taaaluma shuleni hapo.
Mmoja wa wanafunzi hao, Meshak Lonyaki ambaye ni kaka mkuu wa shule hiyo
alisema kuwa walimu wao wamekuwa chanzo cha wao kufeli kwa kutokuwafundisha
darasani badala yake wanadai hela ya kuwafundisha masomo ya ziada(tution) na
kuwatoza shilingi 10,000.
Mbali na hilo pia wanafunzi hao walisema
kuwa katika mtihani wao wa mock ya form two baadhi ya wanafuzi
walirudishwa majumbani kwa kudaiwa michango midogomidogo na kutofanya mitihani
huku baadhi yao wakirudishwa ingawa walilipa lakini muhasibu hakuwaandikia
hivyo kutakiwa kuwasilisha risiti huku wanafunzi wenzao wakiendelea na mitihani
na wengine waliopoteza risiti hawakufanya mitihani.
Katika maelezo yao , Mkuu
wa Mkoa alisema kwamba ni makosa makubwa kwa wanafunzi kukaidi ama kushindwa
kufuata maagizo ya shule hasa yaliyoandikwa katika fomu zao za kujiunga na
shule kwa kufuata masharti ya kulipa ada ambapo aliamuru wakamatwe.
“Askari kamata hawa jamaa weka ndani hawana heshima hata kidogo,haiwezekani
wakaufanya mkoa wa Arusha kama kiwanja cha michezo kwamba kila anayehitaji kucheza
anaruhusiwa kufika, haya mambo hayawezekani hata kidogo, hivyo hawa watakiona
cha mtema kuni na wakome kufika hapa… lazima utaratibu ufuatwe ili kila mmoja
apewe haki ya kusikilizwa”alisema Mkuu wa Mkoa na kuongeza:
“Tena nataka kuchukuwa nafasi hii kupiga marufuku maandamano yote ya
wanafunzi katika Jijini la Arusha, siwezi kukubaliana na suala hili hata
kidogo, kuna viongozi wa serikali wapo shuleni,nyinyi mko huku,Mkuu wa Wilaya
ya Arumeru yuko huko tayari kwa ajili ya kuwasiliza mmekimbilia kwa Mkuu wa
Mkoa tena bila vibali vya maandamano”
Aliishia hapo mkuu huyo bila kutatua kero za wanafunzi hao zaidi ya
kuwakamata waliojieleza, na kuwataka wanafunzi hao warudi shule haraka na
wakichelewa atachukua maamuziya kufunga shule hiyo.
Awali kabla ya wanafunzi hao kufika Ofisi ya mkuu wa mkoa
walikutana na vikwazo vya Askari wa Jeshi la Polisi kwa kupigwa mabomu ya
machozi mfululizo na kusababisha baadhi yao
kujeruhiwa ambapo hata hivyo awali kamanda wa operesheni maalum wa jeshi la
polisi, Peter Mvula alikana wanafunzi hao kupigwa mabomu hadi mmoja wao
alipotoa moja ya bomu ambalo halikulipuka walilorushiwa ndipo walipokubali.
mmoja wa wanafunzi akionyesha moja ya bomu waliloliokota lililorushwa na polisi lakini halikulipuka, ikiwa kama ushahidi kuwa walipigwa mabomu ya machozi |
Maandamano hayo yaliyoanza juzi yana lengo la kumshinikiza Mwalimu
Mkuu wa shule hiyo ya Kinyak aondolewe kwa kile walichodai kwamba anachangia
kudidimiza maendeleo yao
kitaaluma na kwamba anafurahia matokeo mabaya ya wanafunzi hao.
Baada ya Jeshi la Polisi kufanikiwa kuzuia maandamano hayo siku ya kwanza
ya octoba 30 siku inayofuata wanafunzi hao walibuni njia nyingine ya kuandamana
na kufanikiwa kufika katika Ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Arusha pamoja na kupigwa
mabomu ya machozi na kusababisha wengine waliojeruhiwa kurudia njiani.
“Jana Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Nyerembe Munassa alifikia shuleni kwetu
akatuambia kwamba angekuja kesho (yaani leo) kutusikiliza, tukamsubiri hadi saa
nne bila mafanikio ndipo tulipobuni njia nyingine ya kuandamana, tukaamua
kuondoka shule mmoja mmoja mpaka katikati ya mji, ndipo tulipokutana na askari
hao ambapo walianza kuturushia mabomu ya machozi sisi tukawa tunanawa huku
tukiendelea kuja ”alisema Ezekiel Memiri
0 comments:
Post a Comment