Baadhi ya wakazi waliobomolewa nyumba zao wakiwa wamekaa nje |
UNYAMA wa
kutisha umejitokeza katika kijiji cha Sing”isi wilayani Arumeru Mashariki
mkoani Arusha mara baada ya familia tano kubomolewa nyumba zao
kwa amri ya wawekezaji wa kigeni
wanaomiliki mashamba makubwa wilayani humo hali ambayo imepelekea familia hizo kulala nje.
Wananchi
hao wanaishi karibu na shamba kubwa la wawekezaji wa kigeni liitwalo
Mito miwili ambapo hivi karibuni lilivamiwa na wananchi wilayani humo
kwa madai kwamba wanataka wamilikishwe ardhi yao.
Hatahivo,familia hizo zenye wakazi zaidi ya 30 zimeiangukia serikali na kuitaka iingilie kati sakata hilo kwa madai kwamba wanateseka kwa kuishi na hofu ,kukosa chakula sanjari na watoto wao kutohudhuria masomo mashuleni.
Tukio hilo
la kinyama linadaiwa kutokea hivi karibuni majira ya saa 6.30 usiku ambapo
wakiwa wamelala watu ambao wametajwa kuwa ni madalali wa wawekezaji wa kigeni
wanaomiliki mashamba makubwa walivamia katika makazi yao na kisha kuwatoa nje
kabla kabla ya kuanza kubomoa nyumba zao.
Wakizungumza
na waandishi wa habari waliotembelea eneo hilo juzi wakazi hao walisema kwamba
watu hao mara baada ya kuwatoa nje waliwakusanya na kisha kuwafungia katika
chumba kimoja na kisha kuanza kubomoa nyumba zao.
Mzee,Fataeli
Macha pamoja na mkewe Hellen Macha walisimulia kwamba wao ni wakazi halali wa
maeneo hayo tangu miaka ya sitini huku wakisimulia kwamba mbali na kubomolewa nyumba
zao waliporwa mali mbalimbali kama simu,radio,fedha na mali mbalimbali na kisha kutokomea
kusikojulikana.
Kwa nyakati
tofauti wakazi hao walisema kwamba watu hao kabla ya kuanza kubomoa nyumba zao
waliwakuwa wakiwatamkia maneno ya kwamba kwanini wamekataa kulipwa fidia ili
waondoke katika makazi hayo na kisha wwaachie wawekezaji.
“Walikuwa
wanatuambia ya kwamba kwanini tumekataa kulipwa fidia ili tuhame katika makazi
haya na tuwaachie wawekezaji”walisema kwa nyakati tofauti
Naye,Rehema
Mohamed na Amina Idd walisema kwamba watu hao walikuwa wamevalia kofia na
makoti meusi ambapo baadhi yao walipigwa na vitu vizito kabla ya zoezi la
kubomolewa nyumba zao.
Hatahivyo,walimtaja
mtu mmoja aliyetambulika kwa jina la Kileo kwamba ndiye dalali wa wawekezaji wa
kigeni wanaomiliki mashamba makubwa yaliyopo karibu na makazi yao kwamba
amekuwa akiwashawishi wao kupokea fedha za fidia ili wapishe lakini wamekataa.
Walienda mbali zaidi na kusisitiza ya kuwa
mkuu wa wilaya ya Arumeru alifika kuwatembelea na kisha kuwatafutia baadhi yao
nyumba za wageni ili wakahifadhiwe huku wakiitaja taasisi ya Tumaini Foundation
kwamba imewasaidia chakula na msaada wa mashuka.
Mkuu
wa wilaya ya Arumeru,Jeremba Munasa alipohojiwa juu ya tukio hilo
alisema kwamba serikali bado inafanya uchunguzi wa kina juu ya tukio
hilo ikiwa ni pamoja na kuwasaka waliofanya vitendo hivyo.
0 comments:
Post a Comment