Shirikisho
la mchezo wa soka nchini Kenya, Football Kenya Federation (FKF)
limethibitisha kuwa timu ya taifa ya Kenya, Harambee Stars itashiriki
katika michuano ya kuwania kombe la mataifa bingwa kanda ya Afrika
Mashariki na Kati-CECAFA ambayo imepangiwa kuanza tarehe ishirini na
nne mwezi ujao hadi Desemba tarehe nane.
Mwenyekiti
wa FKF, Sam Nyamweya ameyasema hayo hivi karibuni baada ya kukamilisha
mazungumzo na mwenyekiti wa CECAFA, ambaye pia ni rais wa shirikisho la
mchezo wa soka nchini Tanzania, Leodgar Tenga.
Awali
FKF, ilikuwa imetangaza kuwa Harambee Stars haitashiriki katika
mashindano hayo na badala yake itaaangazia michuano ya kufuzu kwa
fainali za wachezaji wanaoshiriki katika ligi za nyumbani barani Afrika
CHAN.
Harambee Stars inajiandaa kuchuana na Burundi baadaye mwaka huu.
Wakati huo huo Nyamweya amesema hawataomba mechi hizo za CHAN kuahirishwa na kwamba Harambee Stars itashiriki kikamilifu.
Harambee
Stars imepangiwa kucheza mechi yake ya kwanza tarehe Mosi Desemba siku
sita tu baada ya kuanza kwa michuano ya CECAFA mjini Kampala na kocha
wa Harambee Stars, atalazimika kuwa na vikosi viwili ili kushiriki
katika mechi zote.
Malumbano makali
yalikuwa yameibuka kati ya viongozi wa soka nchini Kenya na katibu mkuu
wa CECAFA, Wycliffe Musonye, baada ya Kenya kutangaza kuwa haitashiriki
katika fainali hizo kulalamikia uamuzi wa viongozi wa CECAFA wa
kuhamisha mashindano hayo kutoka Nairobi hadi Kampala.
chanzo cha habari: BBC
0 comments:
Post a Comment