Afisa maendeleo ya jamii halmashauri ya Arusha vijijini, bi Mwantumu Dossi alipokuwa akiongea na BERTHA BLOG ofisini kwake hivi karibuni |
Wanawake wametakiwa kusimama kutetea haki zao
wenyewe pindi waonapo zinakiukwa kwa kufuatilia kwenye vyombo vya dola badala
ya kukaa kimya pindi waonapo wanadhulumiwa.
Rai hiyo imetolewa na Afisa
maendeleo ya jamii wa halmashauri ya wilaya ya Arusha vijijini, bi. Mwantumu Dosssi
alipokuwa akiongea na gazeti hili ofisini kwake hivi karibuni.
Mwantumu alisema kuwa
wanawake wengi wamekuwa wakidhulumiwa haki zao lakini hukaa kimya hali
inayowafanya kuteseka kulea familia
(watoto) peke yao
na kusababisha baadhi ya watoto kushindwa kumudu maisha ya dhiki nyumbani na
kukimbilia mtaani.
“Niwaombe wanawake tu
kusimama wima kutetea haki zao pindi waonapo wanadhulumiwa kuliko kukaa kimya
kusubiri mtu akutetee mbali na hilo
pia kujishughulisha na shughuli mbalimbali
za kiujasiriamali kujipatia kipato cha kuwafanya kutokuwa tegemezi” alisema bi
Mwantumu na kuongeza
“Endapo mwanamke ataweza
kupigania haki yake au kujishughulisha na shughuli za kumuingizia kipato
kitaweza kumsaidia kuendelea kulea familia yake pindi mumewe akiwa hayupo au
amefariki lakini akibaki tegemezi atapata shida ya kulea familia na matokeo
yake watoto huchoka maisha ya dhiki na kuamua kukimbilia mtaani na kuongeza idadi
ya watoto wa mitaani” alisema Mwantumu.
Aliongeza kuwa mara nyingi
wanandoa wanapoachana au mwanaume kufariki anayepata shida ya kulea familia ni
mwanamke bila kuambulia chochote cha kumsaidia katika mzigo huo wa malezi peke
yake ambapo wengi wao ni tegemezi wasiopenda kujishughulisha ambapo
amefananisha utegemezi huo kama upumbavu kwa
wanawake kudhika kuwa tegemezi badala ya kujishughulisha na hata biashara ndogo
ndogo.
Akiongelea swala la watoto wa
mitaani bi. Mwantumu alisema kuwa kwa sasa idadi ya watoto wa mitaani inazidi
kuongezeka na sababu kubwa ni mifarakano ya familia na wengine wanatokana na
hali ya uchumi (dhiki) wa majumbani mwao au wengine kuteseka kutokana na kuishi
na watu baki(wasio wazazi wao) hivyo
sababu hizo humfanya mtoto kuona ni bora kutoroka nyumbani na kuingia mtaani
kuomba omba.
Kutokana na hayo Mwantumu
aliiomba jamii kuzingatia maadili, kanuni na taratibu ikiwemo kufuata mila na
desturi za kitanzania kwa kuwasaidia watoto wasio na wazazi au kuwapokea na
kuwalea watoto walioachwa na ndugu zao kwa kufa au kuugua kama wanavyowalea
watoto wao.
Pamoja na bi. Mwantumu
kusisitiza sana
swala la wanawake kutokuwa tegemezi bali wajishughulishe na shughuli za
kiujasiriamali pamoja na kujiunga na SACCOS mbali mbali, pia aliwataka
wanafunzi walioko mashuleni kutokimbilia kuolewa bali wazingatie masomo ili
kujimudu kimaisha hapo baadae.
0 comments:
Post a Comment