BARAZA Kuu la Waislamu wa Tanzania (Bakwata) limetangaza kuwa sikukuu ya
Eid- El- Hajj itakuwa Oktoba 26, mwaka huu. Mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano ya Umma wa Bakwata, Simba Shabani, alisema katika taarifa yake kwa vyombo vya habari kuwa swala la Eid kitaifa itaswaliwa katika msikiti wa Vuchama, tarafa ya Ugweno, wilaya ya Mwanga, mkoani Kilimanjaro na baadaye kufuatiwa na baraza la Eid, litalofanyika msikitini hapo. Alisema mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Rais Jakaya Mrisho Kikwete. Kwa mujibu wa mkurugenzi huyo, jana ilikuwa ni mwezi pili, Dhul- Hijja mwaka 1433, kwa mujibu wa kalenda ya Kiislamu. “Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania, Sheikh Issa Bin Shaabani Simba, anawatakia Waislamu wote na umma kwa ujumla sikukuu njema na kuwataka washerehekee kwa amani na utulivu huku wakichunga mipaka ya Allah (S.W),” alisema.
Na mwandishi wetu-Dar-es-salaam
|
Home
»
»Unlabelled
» WAISLAMU WAJIANDAA NA SIKUKUU YA EID-EL-HAJJ IJUMAA
Friday, October 19, 2012
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment