Waziri wa nishati na madini, Prof. Sospeter Muhongo alipoluwa akiongea na waandishi na habari(hawapo pichani juu ya maazimio ya kikao juu ya maendeleo ya nchi kupitia sekta ya nishati
waandishi wa habari wakisikiliza kwa makini maazimio ya kikao cha nishati kutoka kwa waziri mwenye dhamana (hayuko pichani.
Serikali imeamua
kuwasimamisha kazi kamati ya sekretariet ya nishati kwa lushindwa kufanya kazi
kwa spidi italayoweza kutimiza malengo ya milenia ifikapo mwaka 2015.
Hayo yamebainishwa jijini
Arusha na waziri wa nishati na madini Prof.Sospeter M. Muhongo alipokuwa
akiongea na waandishi wa habari juu ya maazimio yaliyaazimia kwenye kikao cha
siku tatu kilichokuwa kikijadili maswala ya maendeleo ambapo alisema kuwa
wameamua kuwasimamisha sekretariet hiyo kwani wanataka kuboresha uchumi wa
watanzania kupitia sekta ya nishati hivyo kamati hiyo isingeweza kuleta matokeo
mazuri.
Aliongeza kuwa kwa sasa sekta
ya nishati imedhamiria kukuza uchumi wa nchi kwa kuhakikisha wanazalisha umeme
wa kutosha wa kutumika ndani ya nchi kwa kuwasaidia watanzania kuendesha shughuli
za kimaendeleo ambapo pia kunakuwepo na umeme utakaobaki kwa ajili ya kuuza nje
ya nchikukuza uchumi wa watanzani na
Taifa kwa ujumla.
Muhongo alisema kuwa awali
kulikuwepo na tatizo la umeme kutokana na kutegemea chanzo kimoja ambacho ni
maji lakini sasa wanazalisha umeme kwa gesi, mafuta huku maji ikibakia nafasi
ya tatu ambapo kwa sasa pia wanaanza kuzalisha umeme kwa makaa yam awe, nishati
mbadala( jua, joto la ardhi na upepo)
Aidha Muhongo aliongeza kuwa
kupitia mpango huo hadi kufikia mwaka 2020-2025 nchi yetu itakuwa nchi ya
kipato cha kati katika nchi zinazoendelea ambapo uchumi utakuwa ambapo
watanzania watakuwa wakiishi kwa dola kuanzia 4000 hadi 12500 kwa mwaka.
0 comments:
Post a Comment