Kumetokea mlipuko mkubwa katika kampuni ya kutengeneza silaha katika mji mkuu wa Sudan, Khartoum.
Mlipuko
huo ulisababisha moto mkubwa na milipuko zaidi ilifuatia wakati wazima
moto walifika kujaribu kuudhibiti moto huo, uliozuka kutoka kampuni
hiyo ya Yarmouk .
Gaavana wa eneo hilo
(Abdul Rahman Al-Khider Rahman) amesema watu kadha wamepelekwa
hospitalini baada ya kuvuta moshi lakini hakuna aliyefariki.
Amesema
kuwa mlipuko wa kwanza ulitokea katika hifadhi ya silaha na bado chanzo
chake kinachunguzwa. Vifaa vingi vya kijeshi viko karibu na kampuni
hiyo.
chanzo cha habari: BBC
0 comments:
Post a Comment