Hatimaye serikali imeamua kuwachukulia hatua za
kisheria watu wanaohujumu utekelezaji wa mradi wa maji wa kijiji cha Laroi
kilichoko katika kata ya Mateves Wilayani Arumeru.
Akitekeleza zoezi hilo Afisa Tarafa ya Mukulat
Isack Kaserian Maroseck alitoa amri ya kukamatwa kwa mzee Rorian Mesheikini
baada ya mzee huyo anayetuhumiwa kuongoza mgomo huo wa uchangiaji wa mradi wa
maji na uharibifu wa miundombinu ya maji, kukaidi kuhudhuria kwenye kikao cha
mazungumzo na viongozi mbalimbali ngazi ya kata na tarafa ili kumaliza mgogoro
huo.
Mkutano huo ulioitishwa na afisa tarafa hiyo kwa
niaba ya mkuu wa wilaya ya Arumeru Nyerembe Munassa siku ya jumatano katika
ofisi ya kijiji cha Laroi kilimtaka mzee Mesheikini kuhudhuria mkutano huo kutoa
malalamiko yake juu ya mgomo huo wa kuchangia mradi huo wa maji utakaokuwa
ukombozi na msaada mkubwa kwa wananchi wa eneo hilo lakini alikataa ndipo Afisa
huyo kutoa amri ya kwenda kukatwa kwa mzee huyo na polisi.
Aidha mzee Mesheikini na mwenzake ambaye hakuweza
kufahamika kwa haraka walikamatwa na jeshi la polisi oktoba 10 na kupelekwa
katika kituo kidogo cha polisi usa river huku wengine 12 wakiendelea kutafutwa
kwa tuhuma za kukaidi amri ya kikao cha tarehe 29 agost ya kwenda kurejesha
miundo mbinu yote ya maji waliyoharibu.
Isack alisema kuwa Kikao hicho cha tarehe 29
kiliwahusisha polisi, viongozi wa tarafa ya mukulat na kata zote za Tarafa hiyo,
viongozi wa mradi na wananchi wote kwa ujumla na kujadili msaada wa mradi huo
ambapo wote kwa pamoja walikubaliana kuwa wote waliohusika kuharibu miundombinu
hizo za maji warejeshe kwa gharama zao haraka iwezekanavyo ili shirika liendelee
kusambaza maji.
Awali mgogoro
uliibuka katika kijiji hicho baada ya kuletewa mradi wa maji uliojulikana kama
Olmulo development Trust (2003)ambapo wananchi hao walitakiwa kuchangia shilingi
kumi(10)kwa ndoo ya maji ya lita ishirini ili kusaidia ukarabati wa mradi huo
pindi miundo mbinu yake itakapoharibika ua kuchakaa huku mradi huo ukilenga
kusaidia vijiji saba lakini baadhi ya wananchi wa kitongoji cha namba mbili
namba tatu walikaidi hilo wakiongozwa na mzee
Aidha wakielezea madai ya kukataa kuchangia mradi
huo, mzee Mesheikini alisema kuwa hawapo kuchangia mradi huo kwani awali
walikuwa wakitumia maji ya mabomba yaliyowekwa na mkoloni hivyo walitaka
kuendeleza mabomba hayo kwa kuyarepea tu na siyo kuweka mapya.
0 comments:
Post a Comment