Papa Benedict anatuma ujumbe wa maafisa wa Vatican akiwemo askofu mkuu
wa New York, Timothy Dolan -mjini Damascus wiki hii katika juhudi za
kuitaka serikali na upinzani nchini humo kuheshimu haki za binadamu
katika vita vya wenyewe kwa wenyewe vinavyoendelea.
Taarifa
kutoka Vatican zinasema kuwa Papa anatuma ujumbe wa ngazi za juu nchini
humo kuwafariji watu wote wa taifa hilo wanaokabiliwa na wakati mgumu
na wala sio kundi ndogo tu la wakristu.
Waziri
wa mashauri ya kigeni wa Papa, Kadinali Tarcisio Bertone ambaye
ataongoza ujumbe huo amesema kuwa kanisa katoliki haliwezi kushuhudia
tu mkasa nchini syria ukiendelea huku wao wakikaa kimya.
Aidha Mwakilishi wa papa atakutana na viongozi wa serikali na wale wa waasi
.
Mwandishi wa BBC mjini Rome amesema sio jambo la kawaida kwa Vatican kuingilia moja kwa moja katika mzozo kama huo.
Tangazo
hili ambalo ni la ghafla lilitolewa wakati wa mkutano wa maaskofu wa
kikatoliki mjini Vatican na askofu Tarcisio Bertone, ambaye ni naibu wa
Papa ulisema Ujumbe huo unajumuisha waziri wa
mambo ya nje wa Italia pamoja na viongozi wa kanisa hilo kutoka Afrika,
Amerika ya Kusini na Bara Asia wote waliohudhuria mkutano huo hivi karibuni
Viongozi hao watalenga kukutana na pande zote katika mzozo wa Syria, upande wa upinzani na Serikali ya Assad.
Viongozi
wa kikristo nchini Syria walimtumia ujumbe Papa na kumwambia kuwa
wakristo nchini humo wanajipita katika hali ngumu sana.
chanzo cha habari ni BBC.
0 comments:
Post a Comment