mwenyekiti wa mtaa wa Muriet Francis Ndoikai Mbise alipokuwa akiomba halmashauri iwaisaidie kumalizia barabara waliyoianza |
Rai hiyo imetolewa na
mwenyekiti wa mtaa wa Muriet iliyoko kata ya Terrat, Francis Ndoikai Mbisse
jana walipotembelewa na viongozi wa halmashauri katika eneo la ujenzi wa
barabara unaoendelea ambapo alisema kuwa wamekuwa wakiteseka sana kufikia huduma za kijamii
ambazo ziko mbali na maeneo yao kutokana na ubovu wa barabara hasa mvua
zikinyesha ambapo baadhi ya wagonjwa wamekuwa wakipoteza maisha njiani
wakielekea kwenye vituo vya afya kutokana na kuzidiwa kabla ya kupatiwa
matibabu.
“Sisi kama viongozi tuliumia na
hali hiyo pindi tupatapo taarifa hizo ambapo wananchi waliamua kuchangishana
fedha kwa ajili ya ujenzi wa barabara hiyo ambapo waliweza kuchanga fedha za
ujenzi wa barabara hiyo kwa urefu wa kilomita 3 kwa kiwango cha changarawe
lakini mahitaji yalikuwa barabara nzima yenye urefu wa kilomita sita” alisema
Mbisse.
Aliongeza kuwa baada ya wananchi
kuonyesha moyo wa uhitaji wa barabara kwa kuchanga fedha, ujenzi ulianza ambapo
naye meneja wa eneo hili la ujenzi( site manager) Ma Jun kutoka kampuni ya Jiangxi
Geo Engeneering alijitokeza kusaidia nguvu hiyo ya wananchi kwa kutoa lita
200 za mafuta ya greda, vifusi 200 vya changarawe pamoja na greda kwa ajili ya
ujenzi wa bara bara hiyo iliyogharimu zaidi ya milioni 10.
Ma Jun kutoka kampuni ya Jiangxi Geo Engeneering aliyejitolea msaada kwa ajili ya kuwaunga mkono wananchi wa muriet katika ujenzi wa barabara |
“Pamoja na jitihada hizi bado hatujafikia lengo,
hivyo tunaiomba halmashauri yetu itusaidie kumalizia urefu wa kilomita hizo
zingine 3 zilizobaki ili kurahisisha ufuataji wa huduma za kijamii na kupunguza
adha iliyopo sasa ikiwemo wanafunzi kukata tama ya kuhudhuria shule kutokana na
umbali huku hakuna usafiri kutokana na ubovu wa barabara pamoja na watu kufia
njiani wafuatapo huduma mbali.” Alimalizia Mbisse
0 comments:
Post a Comment