Rais wa Marekani Barack Obama, amewatahadharisha wamarekani kuchukulia
kwa uzito kimbunga Sandy huku maafisa wakianza kufunga eneo la
Mashariki mwa pwani ya nchi hiyo wakisubiri kimbunga hicho kupiga.
Majimbo
kadhaa yametangaza hali ya hatari huku mamilioni ya watu wakiathiriwa
na dhoruba kali wakati shule na barabara zikifungwa.
Aidha Wataalamu wanahofia kimbunga hicho huenda kikawa kikali mno wakati kitakapopiga sehemu za nchi hiyo.
Baadhi
ya mikutano ya kisiasa ya hadhara imesitishwa huku Rais Obama akionya
watu kuchukua hatua za kujikinga na athari za zaidi za kimbunga hicho.
Usafiri
wa kimataifa kutoka nchini humo umeathirika sana. Mashirika ya ndege ya
Ufaransa, Uingereza na Virgin Atlantic yamesitisha safari zao katika
baadhi ya sehemu za nchi hiyo ikiwemo miji ya , New York, Baltimore,
Newark, Washington, Boston na Philadelphia kuanzia leo.
Kwa
mujibu wa idara ya utabiri wa vimbunga, saa nane asubuhi ya leo,
kimbunga hicho, kilianza kuelekea Kaskazini kikienda kwa kasi ya
kilomita 760, Kusini Mashariki mwa mji wa New York.
Hali ya tahadhari imetangazwa katika miji ya Maryland, New York, Pennsylvania, Virginia, Washington DC na North Carolina.
Kimbunga
hiki kinatoa fursa kwa Rais Obama kuonyesha uongozi wake mbali na siasa
na ikiwa atakosa kuonyesha uongozi unaostahili huenda wakosoaji wake
wakatumia fursa hiyo kumponda na kumlaumu kwa kosa lolote.
0 comments:
Post a Comment