Kamishna wa madini, Eng. Ally Samaje alipokuwa akiongea na waandishi wa habari(hawapo pichani) juu ya wizi wa madini |
Wamiliki wa migodi hapa nchini
wametakiwa kuwa waaminifu kwa serikali iliyowaamini kwa kuhakikisha wanalipa kodi ili kuongeza
pato la Taifa sambamba na kuisaidia serikali kupata mapato ya kuisaidia kupanga
bajeti zake za maendeleo.
Rai hiyo imetolewa hivi
karibuni mkoani Arusha na Kamishna wa madini hapa nchini, Eng. Ally
Samaje alipokuwa akiongea na waandishi wa habari mkoani hapa.
Alisema kuwa wamiliki wa
migodi kwa sasa siyo waaminifu kutekeleza masharti waliowekewa katika
makubaliano ya uwekezaji katika meneo ya machimbo kwani wengi wao wamekuwa
wagumu kulipa kodi kwa kuwa na visingizio visinyo na tija wala manufaa.
“Kwa sasa serikali imekuwa
ikipoteza mapato mengi katika sekta ya madini kutokana na baadhi ya wamiliki wa
migodi kuiibia serikali kwa kutorosha madini nje ya nchi na kukwepa kulipa kodi
kwa madai kuwa hawajazalisha madini hali inayosababisha hasara kwa Taifa letu”alisema
Samaje.
Aliongeza kuwa kwa sasa
wanaanza mchakato mpya wa kudhibiti hali hiyo kwa kuwadhibiti wahusika
wasitoroshe madini na kama watabainika basi
sheria itachukua mkondo wake, ikiwemo kusitisha mkataba wa uwekezaji na machimbo hayo kurudishwa
kwa serikali ya mtaa.
Aidha aliwataka Watanzania
wasiwapeleke wageni migodini kwa ajili
ya kununua madini bali wathamini Rasilimali zao ikiwemo kwa kutouza madini kwa
mtu (mwenyeji wala mgeni) asiye na lesseni na pia mnunuzi asikubali kununua
madini bila kuwepo kwa risiti ili kuendelea kuwepo na thamani ya madini nchini
kwetu badala ya madini yetu ya Tanzanite kuwa na thamani nchi za nje.
0 comments:
Post a Comment